Jumapili, 27 Julai 2014

Taarifa rasmi kutoka club ya Chelsea kuhusu Didier Drogba.

Screen Shot 2014-07-25 at 9.05.55 PM 
Utakua uliziona tu zile headlines za mitandao na magazeti mbalimbali duniani kuhusu uwezekano wa staa huyu wa soka Didier Drogba kurejea kuichezea Chelsea baada ya Jose Mourinho kuonyesha nia ya kumrudisha.
Sasa taarifa rasmi iliyothibitishwa na Chelsea, mzaliwa huyu wa Ivory Coast amerejea rasmi kwenye club hii kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo wakati akitia saini, Drogba amesema ‘ulikua ni uamuzi rahisi kabisa wa kuamua kufanya tena kazi na Jose Mourinho, kila mmoja anajua uhusiano wangu na hii club… imekua ni kama nyumbani’
Jose Mourinho mwenyewe amesema ‘amerudi kwa sababu ni mmoja wa wachezaji bora Ulaya, namjua vizuri… na amekuja kuiweka historia nyingine’
Drogba ameifungia Chelsea magoli 157 kwenye mechi 342 alizotokezea.
Screen Shot 2014-07-25 at 9.13.00 PM

Video mpya ya Barnaba aliyoonekana na mke wake ndio hii.

Screen Shot 2014-07-26 at 2.30.12 AM
Hii single inaitwa ‘Wahaladee’ ambayo ni miezi kadhaa imepita tangu utoke rasmi kwenye Radio lakini July 25 2014 Watanzania wameletewa video yake ambayo imeongozwa na Nick Dizzle ambapo kingine kikubwa kwenye hii video ni mrembo alieigiza ndani yake, ni mke wa ndoa wa Barnaba (Mama Steven)
Naambiwa video imefanywa Kenya na Tanzania.

Matokeo ya tuzo za AFRIMMA 2014 alizokua anawania Diamond Marekani.

Screen Shot 2014-07-27 at 9.43.50 AM 
Zinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news za ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja Babu Tale ambae nae kahudhuria tuzo hizi Marekani alienitumia msg kwa kusema Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.

Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.01 AM 
Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Producer bora wa mwaka tuzo yake imechukuliwa na Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.33 AM
Tuzo zenyewe zimetolewa kwenye hili jengo
Stori zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo endelea kukaa karibu na millardayo.com mtu wangu ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili ambalo limewahusisha wakali wengine kama Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour, Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.

Dully Sykes anakualika kusikiliza single yake mpya hapa inaitwa ‘Togola’

Dully Sykes 1
Mara yake ya mwisho kusikika na single mpya kwenye Radio ilikua June 2013 na ilikua ni ‘Kabinti special’ ambayo video yake ilionekana ndani ya muda mfupi sana toka iachiwe na hiyo ni kutokana na video hiyo kutajwa kwamba haijazingatia maadili ya Kitanzania kuonyeshwa hadharani.
Sasa leo Dully anayofuraha kutualika kusikiliza single yake mpya inaitwa ‘Togola’ ambayo baada ya kuisikiliza unaweza kuacha maoni yako kwenye comment hapa chini ili akipita baadae jioni asome kutoka wa watu wake.

AJARI YA GARI WALIYOPATA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJIRI AKIWEMO BAHATI BUKUKU.

Screen Shot 2014-07-26 at 9.57.39 PM 
Gari lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31) mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine linalosadikiwa kuwa Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David  Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.
Waliojeruhiwa ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mwingine ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.
Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.
 Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.

Ijumaa, 25 Julai 2014

KAMPENI YA UGAWAJI WA VYANDARAU VYA HATI PUNGUZO

imagesWizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeandaa kampeni kwa ajili ya ugawaji wa vyandarua vya hati punguzo katika kaya nchini, inayotarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Dkt Kebwe Stephen, amesema kampeni hiyo imeanzishwa ili kuziba pengo kutokana na kusitishwa kwa huduma ya hati punguzo iliyokuwa ikifadhiliwa na Mennonite Economic Development Associates (MEDA) mapema mwezi Juni 2014 .

Dkt. Kebwe aliongeza kuwa  jamii pamoja na wakina akinamama wajawazito watanufaika na kampeni hiyo, ikiwemo ile ya  ugawaji wa vyandarua kwa wanafunzi shuleni ambayo imeanza kutekelezwa tangu mwaka 2013 kwa mikoa ya Lindi,Ruvuma na Mtwara.

“kampeni hii ni muhimu na ni mojawapo ya njia mbadala ya kuendelea kuwasaidia akinamama wajawazito na watoto wachanga kujikinga na ugonjwa wa malaria ikiwa ni mkakati wa kupunguza vifo vya akinamama na watoto”alisema Mhe.Dkt. Kebwe

Aidha, jumla ya vyandarua milioni 13 vimesambazwa kupitia mpango huo, ambapo imechangia katika kuongeza matumizi ya vyandarua kwa akinamama wajawazito  kutoka 16%  mwaka 2004 hadi 75% mwaka 2012 na kutoka 16% hadi 76% kwa upande wa watoto.

Pia alifafanua kuwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua itaendelea kutolewa Kwa watumiaji wa vyandarua hivyo, kwani baadhi ya watu wamekuwa wakitumia tofauti kwa kufugia kuku na hata wengine kuweka katika bustani ili kukinga ndege waharibifu badala ya kujikinga na mbu.

Mpango huu wa hati punguzo ni mkakati ulioendelevu kuhakikisha kuwa makundi ya akinamama wajawazito na watoto wachanga wanaendela kupata vyandarua ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa malaria na umekuwa ukitekelezwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Kifua kikuu na Malaria, Shirika la Maendeleo la Serikali ya Watu wa Marekani (USAID), Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) na Idara ya Maendelao ya nchi ya Uingereza

Alhamisi, 24 Julai 2014

Ban Ki Moon asema Iraq inapaswa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

Parliament elected Masum, who served as the first PM of Iraq's autonomous Kurdish region more than two decades ago, by an overwhelming majority of 211 votes to 17.
Watu waliokuwa na silaha wameushambulia msafara uliokuwa umewabeba wafungwa kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, na kusababisha makabiliano makali na majeshi. Wafungwa zaidi ya 50 na wanajeshi kumi wameuawa katika shambulizi hilo lililodhihirisha hali ya kutokuwa na amani nchini Iraq. Hii ni hata baada ya wabunge kumchagua leo mwanasiasa kigogo wa Kikurdi Fouad Massoum kuwa rais mpya. Massoum mwenye umri wa miaka 76, alipata kura 211 kati ya 228 na sasa anachukua nafasi ya Jalal Talaban ambaye mihula yake miwili ya uongozi wa miaka kumi imekamilika. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon aliwasili nchini humo mapema leo akiwaomba wabunge "kutafuta msimamo wa pamoja" ili waweze kuutatua uasi unaofanywa na kundi la itikadi kali za kiislamu linalojiita Dola la Kiislamu, pamoja na wanamgambo wa Kisunni ambao wameiteka miji kadhaa ya kaskazini na magharibi mwa Iraq. Akizungumza pamoja na Waziri Mkuu wa Iraq Nuri al-Maliki, Ban amesema Iraq inakabiliwa na "kitisho kikubwa, lakini kinachoweza kutatuliwa kama itaunda serikali inayowahusisha viongozi wa matabaka mengi.

Ndege ya abiria ya Algeria yaripotiwa kuanguka kaskazini mwa Mali


Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa.
Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
„Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa.Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua"

Ameongeza kuwa waziri wa ulinzi wa ufaransa alikuwa akisaidia katika utafutaji wa ndege hiyo.
"Waziri wa ulinzi wameviruhusu vyombo vyao kwenda kwenye eneo kuitafuta ndege. Majeshi ya Algeria na Umoja wa mataifa wanafanya hivyo pia. Ndege mbili za jeshi la ufaransa zilizopiga kambi Niyame hivi sasa na tangu asubuhi zimekua zikiitafuta ndege hiyo. Majeshi yetu katika eneo hilo ikiwamo vifaa vya matibabu vyote viko tayari"

Hapo awali, waziri mkuu wa Algeria Abdelmalek Sellal alitoa ufafanuzi wa tukio la kuanguka kwa ndege hiyo.
"Usiku wa jana kama saa 9 ndege ya Hispania iliyokodiwa na Shirika la Ndege la Algeria ilikuwa katika safari yake kati ya Ouagadougou na Algiers. Ilipoteza mawasiliano na Rada muda huo wa saa tisa usiku dakika 10 tu baada ya kupaa. Mawasiliano ya mwisho ilikuwa na mnara wa kuongozea ndege ulioko Niger na ndege ilikuwa juu ya Gao, kama kilomita 500 kutoka kwenye mpaka wa Algeria. Kulikuwa na abiria 119 wakiwamo wafanyakazi wake. Utafutaji bado unaendelea na tunawasiliana na mamlaka zinazohusika. Waliokuwa kwenye ndege ni raia wa Algeria pamoja na mataifa mengine"

Mamlaka zinazohusika nchini Burkina Faso ambako ndiko ndege ilitokea wameamua kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia wa wale waliokuwa katika ndege. Baadhi ya ndugu wamefika katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou kufuatilia taarifa kuhusu ndugu zao. Baadhi walikuwa na malalamiko
"Tuwanataka watuambie kama ndege hiyo imeanguka, kuna walionusurika, au wote wamekufa. Hayo ndio tunayotaka kujua. Tupo kwenye wakati mgumu. Watatu miongoni mwetu, tulitaka kusafiri na dada yetu lakini tuliamua kuahirisha safari katika dakika za mwisho. Hata hivyo dada yetu yeye aliondoka usiku jana."
Mwaume mwingine aliyekuwepo kwenye uwanjahuo wa ndege alisema.

Mnigeria aliebeba dawa za kulevya alivyokamatwa Nairobi baada ya rubani kuugua.

Nairobi-Kenya-International-AirportMwanamume mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na mzigo wa dawa za kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake.
Huyu jamaa alikua anazisafirisha hizi dawa kutoka Lagos kwenda Bangkok lakini ghafla akaanza kupata maumivu baada ya kuchelewa kufikisha mzigo aloubeba tumboni mwake baada ya ndege waliyokua wakisafiria kutua Nairobi kwa dharura.
Ilitua kwa dharura baada ya rubani kuumwa ghafla hivyo kulazimu ndege kutua Nairobi kisha abiria wote kupelekwa hotelini na hapo ndio Mnigeria huyu akaanza kuhisi maumivu makali tumboni.
Aeroplane landing at sunset, CanadaSimon Ithae ambae ni mkuu wa mawasiliano hospitali ya Kenyatta amesema ‘alitueleza amemeza vidonge na alikua akiamini ndicho chanzo cha maumivu hivyo alipoona hawezi kustahamili aliita Polisi akidai ameumizwa na anahitaji kupelekwa hospitali lakini lengo lake ni apange njama na madaktari kutoa dawa za kulevya bila yeye kukamatwa na aendelee nazo na safari lakini mipango yake haikufanikiwa kwa sababu Madaktari walimpa chakula ili kutoa dawa hizo na kisha wakawapa taarifa Polisi.

Mwanamke wa Sudan aliehukumiwa kifo kwa kuolewa na Mkristo amewasili Italia.

Sudan 1
Huyu wa kwanza kushoto aliembeba mtoto ni Makamu wa waziri wa mambo ya nje ya Italy Lapo Pistelli
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis Alhamisi ya July 24 2014 nchini Italia amekutana na Meriam mwanamke wa Sudan ambae alihukumiwa kunyongwa nchini Sudan kwa kosa la kuolewa na mume Mkristo mwaka 2011.
Meriam na watoto wake wawili akiwemo huyu wa mwisho aliezaliwa gerezani pamoja na mume wake ambae ni raia wa Marekani mwenye asili ya Sudan, waliwasili Italy wakiwa wameongozana na Afisa wa Italia ambae alisaidia kwenye mazungumzo na serikali ya Sudan ambayo iliwashikilia Meriam na mumewe kwa wiki kadhaa baada ya kuwakamata Airport wakiondoka nchini humo.
Video iliyotolewa na Vatican imemuonyesha Pope akimpa Meriam medali pamoja na rozari ambapo baada ya kukutana na Pope, wawili hawa wakiwa na watoto wao watambatana kuelekea nchini Marekani ambako ndiko makazi yao yalipo New Hampshire alikowahi kuishi mume wa Meriam.
New Hampshire Marekani.
New Hampshire Marekani.
Afisa wa Italia aliehusika kuongea na serikali ya Sudan ili familia hii iachiwe, amesema ilibidi wawe wapole kwenye maongezi na ndicho kilichosaidia mwishoni wakaachiwa huru baada ya kushikiliwa pamoja na kwamba Mahakama kuu ya Sudan ilimuachia huru Meriam.
MS3
Meriam mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifo baada ya kukataa amri ya kurudi kwenye dini ya baba yake ambae ni Muislamu ambapo alifungwa gerezani na kujifungulia mtoto wake wa pili hukohuko akiwa amefungwa minyororo mpaka miguuni wakati wa kujifungua.
sudan 3
Waziri wa mambo ya nje wa Italia Federica Mogherini akiwa na mtoto wa Meriam wakati wakiwasili nchini Italy July 24 2014 baada ya kuachiwa huru Sudan.

Ratiba ya Serengeti Fiesta 2014 imetoka mdau wangu..

fiestaa
Fiesta ni tamasha linalowakutanisha wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania kwenye msimu wa mafanikio pamoja na mashabiki wao kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kuna mikoa kadhaa imeongezeka.
Kupitia show ya XXL, Sebastian Maganga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta 2014 amesema mwaka huu kuna mikoa minne imeongezeka lakini kwa utangulizi kwa kanda ya ziwa imeongezeka Kahama na Bukoba.
Fiesta 2014 itaanzia Mwanza August 09 kisha wiki ya pili ni Bukoba ambayo itakua August 15 na Kahama August 17 baada ya hapo ni Musoma August 22 na Fiesta 2014 kwa kanda ya ziwa itamaliziwa Shinyanga Mjini August 24.
SERENGETI 2014 TUPO PAMOJA, SAMBAZA UPENDO..  NI HATAREEE.

NDEGE NYINGINE YAPOTEA HUKO ALGERIA



Maafisa wa masuala ya anga nchini Algeria wanasema wamepoteza mawasiliano na ndege ya shirika la ndege la Air Algerie, iliyokuwa katika anga ya Sahara. Shirika la habari za Algeria limesema ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda Algiers na kupotea kwenye rada takriban dakika 40 baada ya kupaa kutoka jijini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso. Air Algerie imesema imeanza shughuli za dharura kuitafuta. Indadhaniwa kuwa na abiria 110 na wafanyakazi sita. Njia ya ndege hiyo ni kupitia nchini Mali ambapo kuna mzozo unaendelea upande wa kaskazini.

Photo: NDEGE NYINGINE YAPOTEA
Maafisa wa masuala ya anga nchini Algeria wanasema wamepoteza mawasiliano na ndege ya shirika la ndege la Air Algerie, iliyokuwa katika anga ya Sahara. Shirika la habari za Algeria limesema ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda Algiers na kupotea kwenye rada takriban dakika 40 baada ya kupaa kutoka jijini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso. Air Algerie imesema imeanza shughuli za dharura kuitafuta. Indadhaniwa kuwa na abiria 110 na wafanyakazi sita. Njia ya ndege hiyo ni kupitia nchini Mali ambapo kuna mzozo unaendelea upande wa kaskazini.

TETESI ZA SOKA ULAYA

Liverpool wapo tayari kumfuatilia tena Ryan Bertrand, 24, kutoka Chelsea, wakati Brendan Rodgers akisaka beki wa kushoto (Daily Mail) kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, na beki wa Southampton Dejan Lovren, 25, ni miongoni mwa wachezaji Brendan Rodgers anawafuatilia (Daily Mirror) Everton wanakaribia kumsajili Muhamed Besic, 21, kutoka Bosnia (Daily Mirror), Tottenham wanafikiria kumtaka beki Ron Vlaar, 29, wa Aston Villa, na wapo tayari kubadilishana na Lewis Holtby au Michael Dawson (Daily Mail), Chelsea wanamfuatilia kwa karibu beki Rafael Varane kutoka Real Madrid (Independent), Liverpool wana matumaini ya kuuteka mchakato wa uhamisho wa kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, kwa kutoa dau la pauni milioni 42.5 walizotoa Manchester United (Metro), meneja wa Everton Roberto Martinez amethibitishwa kuwa anakaribia kumsajili David Henen, 18, kutoka Anderlecht (Talksport), AC Milan wanamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal, Joel Campbell, 22, na tayari wamewasiliana na klabu hiyo ya London (Inside Futbol) Louis van Gaal anakabiliwa na mtihani mgumu baada ya Borussia Dortmund kumuonya kuwa asahau kumsajili Mats Hummels, 25 (Daily Express), Manchester United 'wameruhusiwa' kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26, baada ya timu hiyo kumsajili James Rodriguez kutoka Monaco (Caughtoffside) hata hivyo taarifa nyingine zinasema Di Maria anataka kwenda PSG kwa mkopo kwanza kabla ya uhamisho wa kudumu msimu ujao (Daily Express), boss wa Chelsea Jose Mourinho amewaambia makipa wake, Thiabaut Courtois, 22, na Petr Cech, 32, kuwa hawaendi popote, watake wasitake (Times), Arsene Wenger yuko tayari kuacha kutafuta kiungo mwingine, na atamuamini Jack Wilshere, 22 (Daily Mirror), boss wa QPR, Harry Redknapp anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o (Daily Mirror) Romelu Lukaku wa Chelsea, 21, anakaribia kuondoka Darajani baada ya kufanya mazoezi na klabu yake ya zamani Anderlecht (Sun). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Like na share kwa wingi hili kuongeza ushirikiano.

Sakata la Viungo vya Binadamu kutupwa Dar, Chama cha Madaktari chataka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) Kifungwe

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU)  sanjari na hospitali iliyo chini yake, vinastahili kufungiwa.
 
Tamko hilo la chama limekuja huku mamlaka mbalimbali zinazohusika na usimamizi wa karibu wa vyuo vikuu vya matibabu zikikiweka chuo hicho kiporo,  kusubiri uchunguzi wa tuhuma zinazokikabili za kutupa viungo vya binadamu jalalani, ukamilike kabla ya kuchukua hatua zinazostahili.
Kitendo hicho cha kutupa viungo vya binadamu jalalani kimetajwa na watu mbalimbali, wakiwemo wataalamu kuwa ni cha  ajabu kinachodhalilisha nchi na utu wa binadamu.
 
Rais wa MAT, Dk Primus Saidia alisema kitendo hicho  ni cha aibu na kwamba  kama ingekuwa nchi nyingine, walistahili kufungiwa
 
http://www.gumzolajiji.com/wp-content/uploads/2014/07/MAITI.jpg
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, alisema taasisi hiyo isingetakiwa kutoa mafunzo ya udaktari wala kufanya tafiti zozote, ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kutoa huduma za afya  katika hospitali yake.
 
Mwingine aliyezungumzia sakata hilo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Margareth Sitta aliyepongeza taasisi za serikali kwa hatua za haraka walizochukua kuhakikisha watu hao wanabainika mapema na kukamatwa.
 
Hata hivyo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa nyakati tofauti, walisisitiza nia yao ya kuchukua hatua dhidi ya chuo hicho, mara jopo linalochunguza sakata hilo litakapokamilisha kazi yake. 
 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Kebwe Stephen alisema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho ambacho si cha kawaida.
 
Alitaka  upelelezi ufanyike haraka, adhabu stahiki ichukuliwe kutokana na kitendo hicho.
 
 “Baada ya kukamilika kwa upelelezi wa tukio hili na kupata taarifa za kwa nini walifikia hatua hii, naahidi wizara yangu itachukua hatua kali,” alisema Kebwe.
 
Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es  Salaam jana, msemaji  wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja alisema kutokana na kuwa jambo hilo ni jipya, wataangalia uwezekano wa kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
Alisema ingawa wizara yake haihusiki na usimamizi wa vyuo hivyo vinavyozalisha madakatri na kutaka waulizwe TCU, kwa mujibu wa Mwamwaja, kitendo walichofanya madaktari husika si cha kimaadili.
 
Alisema pamoja na kuwa kitendo hicho si cha maadili pia wanaangalia madhara ya kiafya kulingana na tukio hilo.
 
“Lakini pia ni vema kuangalia na jiji (Dar es Salaam) ni jinsi gani wanasimamia madampo yao, kwa nini inaruhusu kumwaga uchafu wowote bila kuwepo wakaguzi au ni utaratibu gani wanatumia kulinda afya za wananchi,”alisema  Mwamwaja.
 
Kwa upande wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yenye dhamana na vyuo vikuu, Katibu Mkuu wake,  Profesa  Sifuni Mchome alisema pia wanasubiri ripoti  ya timu iliyoundwa kuchunguza suala hilo wachukue hatua za haraka chini ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
 
“Kwa sasa uchunguzi unaendelea hivyo hatuwezi kuchukua hatua yoyote,” alisema Profesa Mchome. Katibu Mkuu alisema katika tume hiyo iliyoundwa na polisi, yumo  mwakilishi wa elimu kutoka TCU.
 
Alisisitiza wataangalia suala hilo na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kwa sasa hakuna sheria inayowabana kutokana na kuwa suala hilo ni jipya nchini.
 
Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Habari Mwandamizi wa TCU, Edward Mkaku alisema wanasimamia ubora wa elimu ya juu na suala lililotokea ni kesi ya chuo kwa asilimia 100.
 
Hata hivyo, alisema kwa kuwa Mkurugenzi wa Ithibati wa Elimu ya Juu katika tume hiyo yupo kwenye tume iliyoundwa, wataangalia hatua za kuchukua baada ya uchunguzi kukamilika.
 
Alisema TCU ni taasisi yenye utaratibu, hivyo itatoa uamuzi baada ya ripoti kwa kuwa sasa IMTU bado ni watuhumiwa na haipaswi kuhukumiwa.
 
“Tunasubiri tume imalize uchunguzi ndipo tutaona tutachukua hatua gani kulingana na  Sheria ya Vyuo Vikuu kwani kwa sasa sheria ya suala hilo haipo kutokana na kwamba ni jipya kutokea nchini,”alisema.
 
Wakili wa Kujitegemea kutoka MK Law Chambers, Karoli Mluge akizungumza nafasi ya sheria katika suala hilo, alisema hakuna sheria inayozungumzia kwamba kutupa viungo vya binadamu au mwili hadharani ni kosa.
 
Mluge alisema  jamii lazima itofautishe Sheria na suala zima la maadili na ubinadamu. Alisema kibinadamu na maadili, utupaji wa viungo vya binadamu si sahihi na ni jambo linaloshitua lakini  kisheria, haimtii mtu hatiani .
 
“Kimaadili si sawa, lakini suala hili ni la kiubinadamu  halina sheria,” alisisitiza. Alisema hata mtu anapokutwa na kiungo cha binadamu, hatiwi hatiani kwa maana ya kukutwa na kiungo husika isipokuwa, kinachotafutwa ni kujiridhisha ni kwamba amekipataje kutoka mwili wa binadamu.
 
“Si kosa kukutwa na kiungo cha binadamu…cha msingi, ni kuthibitisha umekipataje,” alisema. 
 
Kumekuwepo maswali juu ya ni namna gani vyuo vinapata miili ya kufanyia mafunzo kwa vitendo na baada ya mafunzo inapaswa iteketezwe namna gani. Hata hivyo katika kutafuta ufafanuzi wa maswali haya, taasisi hizo zinazohusika na usimamizi wa vyuo hazikuwa tayari kuzungumzia kwa undani suala hilo, kwa madai ya kusubiri matokeo ya tume iliyoundwa.
 
Tume hiyo iliyoundwa, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, itahakikisha inakuja na majibu, ikiwa ni pamoja na kujua idadi kamili ya watu wenye viungo hivyo.
 
Timu hiyo ya wataalamu ya watu saba inayohusisha pia Mkemia Mkuu wa serikali, itakuja na majibu viungo hivyo ni vya muda gani na zilitumika kemikali gani kuvikausha.
 
Jopo litabaini pia  kama ipo sheria na ni ipi  inavunjwa. Inalenga kubaini pia kama upo uzembe katika kulinda viungo vya binadamu na vinapatikanaje kwa ajili ya mazoezi.
 
Katika sakata hilo lililovuta hisia za watu na kuzua mjadala mitaani na kwenye mitandao ya kijamii, watu wanane wakiwemo Madaktari wa IMTU, walikamatwa juzi na Polisi kwa mahojiano wakituhumiwa kuhusika  katika  utupaji viungo vya binadamu jalalani.
 
Polisi ilisema mifuko ipatayo 85 yenye vichwa, miguu, mikono, moyo, mapafu, vifua na mifupa ya aina mbalimbali ya binadamu, ilikutwa maeneo ya bonde la Mbweni Mpiji, eneo la Bunju jijini Dar es Salaam.

Binti wa SUDAN aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya UISLAMU ahamishiwa ITALIA

Meriam Ibrahim akiwa na mumewe Daniel Wani pamoja na mtoto wao wa kwanza.Meriam Ibrahim akiwa na mumewe Daniel Wani pamoja na mtoto wao wa kwanza.
MWANAMKE wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya Kiislamu na kuolewa na Mkristo, Meriam Ibrahim, amesafirishwa kuelekea Italia baada ya kukaa ubalozi wa Marekani mjini Khartoum, Sudan kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Meriam na familia yake wameondoka na ndege ya Serikali ya Italia wakisindikizwa na Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Lapo Pistelli.
Awali Meriam alihukumiwa kifo na viboko 100 baada ya kuasi dini ya baba yake ambaye ni Muislamu na kuolewa na Mkristo, Daniel Wani.
Baadaye mwanamke huyo alifanikiwa kuachiwa huru baada ya wanaharakati kuingilia kati japo alikamatwa tena kabla ya kuachiwa na kukaa katika ubalozi wa Marekani, Khartoum.

Kiiza, Okwi, Twite, Niyonzima, nani kumpisha mbrazil Genilson Santos ‘Jaja’ Yanga?


Kuwasili kwa wabrazil wawili katika klabu ya Yanga kumeweka rehani ajira za wachezaji Emmanuel Okwi, Hamis Kiiza, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima kwasababu mmoja wao inabidi atemwe ili timu hiyo iweze kutimiza masharti ya kuwa na wacheza kigeni watano tu.
Lakini kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba Kiiza ndio atatemwa na kumpisha mshambuliaji  Genilson Santos ‘Jaja’ ndani ya listi ya wachezaji wa kigeni.
Mwanaspoti linaripoti – YANGA ipo katika mchakato wa kuachana na Hamis Kiiza (pichani)  ili nafasi yake achukue Genilson Santos ‘Jaja’, lakini hawajamwambia chochote na hata wakizungumza nae wanazuga tu kama hamna kitakachotokea.
Pia straika huyo wa Uganda ameshashtukia dili na amesema kwamba hana wasiwasi wowote kuhusu hilo na anangoja kauli ya viongozi wake, ingawa Mwanaspoti linajua kwamba Simba wanamnyatia na SC Villa ya Uganda imeshafanya nae mazungumzo ya awali wanasubiri Yanga impe chake wamnase.
Hadi sasa Yanga ina mkataba na wachezaji sita raia wa kigeni lakini kanuni za Ligi Kuu ya Bara inaelekeza matumizi ya wachezaji watano tu wa kigeni, hivyo inalazimika kuachana na mmoja wa wanasoka hao.
Wachezaji wa kigeni wa Yanga ni Kiiza na Emmanuel Okwi (wote Uganda), Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite (wote Rwanda), Jaja na Andrey Coutinho wote kutoka Brazil.
Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema mmoja kati ya Okwi na Kiiza anatakiwa kuachwa lakini kura inaonekana kumuangukia Kiiza ambaye sasa yupo katika kikosi cha Uganda ‘The Cranes’ akijiandaa na mechi ya marudiano ya Kombe la Afrika dhidi ya Mauritania.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Uganda, Kiiza alisema; “Kama Yanga wamepanga kuniacha waniambie tu haina shida, halafu nitajua jambo la kufanya. Sihofii lolote kuhusu uamuzi utakaochukuliwa na viongozi kwa maana soka ni ajira yangu.”Kiiza alisema mkataba wake unaisha Mei mwakani hivyo kama Yanga ikitaka kuachana naye itabidi ivunje naye mkataba.
“Naamini bado nina uwezo mkubwa na nimeweza kuifanyia mambo mengi Yanga hivyo sina wasiwasi kama wataniacha nitakuwa sehemu nyingine lakini kwa sasa naheshimu mkataba wangu na Yanga kwani ni timu mwajiri wangu.”Na mwanamichezo wako Nickson Luvega.

Magazeti ya leo July 24 2014

.
.
Kama kawaida youngluvega.blogspot.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.