Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam inawashikilia watuhumiwa wawili wa ujambazi ambao wanahusishwa na mauaji ya Mtawa wa Kanisa Katoliki Sista Clezensia Kapuli.
Mbali na watuhumiwa hao pia watu wengine sita wanashikiliwa wakihusishwa na matukio mbali mbali ya ujambazi hapa nchini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova, amewataja majambazi wanaohusishwa na mauaji ya Sista huyo kuwa ni Manase Ogenyeke “mjeshi” (35) mkazi wa Tabata Chang’ombe na Hamis Shaban “Carlos” mkazi wa Magomeni mwembechai.
Wengine waliokamatwa kutokana na matukio mengine ya ujambazi ni Beda Mallya miaka (37) mkazi wa Mbezi msakuzi, Michael Mushi (50), Sadick Kisia (32), Elibariki Makumba (30), Nurdini Suleiman (40) pamoja na Mrumi Salehe (38).
Majambazi hao wamekamatwa kutokana na Operesheni inayoendelea jijini Dar es Salaam baada ya kifo cha Mtawa huyo kilichotekea Juni 23 mwaka huu, kamanda Kova amesema majambazi hao wawili pia wanahusika na tukio la uporaji fedha katika Benki ya Barclays tawi la Kinondoni lililotokea miezi michache iliyopita.
Jumatano, 2 Julai 2014
Home »
» Kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya Sista aliyepigwa risasi Ubungo.
Kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya Sista aliyepigwa risasi Ubungo.
Related Posts:
Hiki ndicho alichokiongea yule Msichana aliyempiga Mtoto Uganda. Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo. Msichana hu… Read More
Picha ya kwanza ya mbrazil mpya wa Yanga mazoezini, je atafuzu majaribioWiki iliyopita nilikuletea taarifa juu ya ujio wa mchezaji mpya wa kimataifa wa klabu ya Yanga Emerson de Oliveira Neves Roque – mbrazil ambaye ameletwa nchini kuja kufanya majaribio na endapo ikifuzu basi ndio itac… Read More
Baada ya ishu ya Escrow, haya ni majibu mawili ya Waziri Mkuu Pinda ikiwemo kujiuzulu Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda. “…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa T… Read More
Kilichosemwa na Kamanda Kova na Waziri Lazaro Nyalandu kuhusu ajali ya Helikopta Taarifa ambayo imeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni kuhusu watu wanne kufariki kutokana na ajali ya Helikopta inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye namba 5HTWA kuanguka katika eneo la Kipun… Read More
Mnigeria mwingine kwenye hatia ya kusafirisha dawa za kulevya Idadi ya raia wa Nigeria wanaokamatwa na dawa za kulevya inazidi kupanda siku hadi siku, ambapo taarifa iliyopo ni kwamba mtu mmoja mwenye umri wa miaka 35 amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kusafiri… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni