Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO) enzi za uhai wake
Jeneza lenye mwili wa marehemu Daniel Lema kabla ya kuagwa.
Marehemu Daniel Lema akiwa hospitali baada ya kuchomwa moto na wananchi.
Ndugu wa marehemu wakiandaa jeneza kwa ajili ya mwili wa marehemu Daniel kuagwa.
Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College - RUCO), amefariki dunia baada ya kushambuliwa kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira akidhaniwa kuwa mwizi.
Tukio hilo lilitokea Juni 24, 2014, majira ya saa 5 usiku ambapo inadaiwa kuwa Daniel alikuwa ametoka kuangalia michuano ya Kombe la Dunia, akawa anatafuta chakula cha jioni ambapo alipofika kwenye mgahawa mmoja ambao ulikuwa umefungwa, aliingia ndani ambapo binti aliyekuwa amelala ndani ya mgahawa huo, alianza kupiga kelele za mwizi zilizowakusanya wananchi wenye hasira kali.
Wananchi hao walianza kumshambulia Daniel wakiongozwa na mlinzi mmoja wa jamii ya Kimasai, baada ya kuzidiwa na kichapo wananchi hao walimmwagia mafuta ya taa na kumchoma moto kisha wote wakatoweka.
Mwanafunzi huyo aliokolewa na madereva bodaboda ambao walizima moto na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa lakini siku kadhaa baadaye alifariki dunia.
Mwili wa marehemu umeagwa mapema leo katika hospitali hiyo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Jumatano.
Mungu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA
Jumanne, 1 Julai 2014
Home »
» JE WAJUA MWANAFUNZI CHUO KIKUU ALIYECHOMWA MOTO AFARIKI, KUZIKWA KESHO KILIMANJARO
JE WAJUA MWANAFUNZI CHUO KIKUU ALIYECHOMWA MOTO AFARIKI, KUZIKWA KESHO KILIMANJARO
Related Posts:
JESHI LA KENYA LAFANYA SHAMBULIO SOMALIA Ndege za kijeshi za Kenya zashambulia Somalia Jeshi la Kenya limeshambulia maeneo mawili ya jimbo la Gedo nchini Somalia,ambalo ni makao ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab,ikiwa ni s… Read More
SHAMBULIZI GARISSA:SERIKALI YAJITETEAWilliam Ruto Serikali ya Kenya imeitetea idara yake ya usalama kufuatia shutma kwamba ilichelewa kukabiliana na shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa. Shambulio hilo lilisitishwa baad… Read More
Chelsea yashinda huku Costa akijeruhiwaDiego Costa akianguka katikakati ya wachezaji wa stoke city Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa ilikuwa hatari kumchezesha mshambuliaji Diego Costa baada ya kujeruhiwa wakati wa ushindi wa Chelsea wa… Read More
Nimekuwekea matokeo ya EPL hapa, yakiwemo ya Man UTD vs Sunderland Baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyo ya kuridhisha katika ligi kuu ya England tangu kuanza kwa mwaka 2015, klabu ya Manchester United leo iliwakaribisha kwenye uwanja wao wa nyumbani Sunderland. Mchezo huo wa ra… Read More
Waziri MEMBE amesema huu ni mchango wa Marehemu Kapteni KOMBA kwenye mgogoro wa Ziwa Nyasa Leo ni siku ambayo mwili wa Marehemu Kapteni John Damian Komba umepumzishwa katika makaburi ya Kijijini kwao Lituhi, Mbinga mkoa wa Ruvuma. Leo kwenye kipindi cha Power Breakfast Clouds FM, alisikika Waziri wa Ma… Read More
0 comments:
Chapisha Maoni