Alhamisi, 17 Desemba 2015

Rais Magufuli: Kwa Mara ya Kwanza Serikali Inakusanya Takribani Trilioni 1.3 Kwa Mwezi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amesema kwa mara ya kwanza Serikali itakusanya takribani trilioni 1.3 kwa mwezi. Pia amewahakikishia watanzania kuwa ahadi yake ya kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ni lazima itekelezwe. Amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kazi nzuri...

Nyimbo 5 za Diamond zilizopo Store Zitaendelea Kumuweka Kileleni kwa Miaka 10 – Asema Mpiga Picha Wake

Diamond Platnumz ni msanii ambaye (angalau kwa sasa) haoneshi dalili za kushuka kimuziki hivi karibuni. Tunayo mifano mingi ya wasanii wa Bongo ambao waliwahi kufanya vizuri sana na baadaye kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki. Diamond ambaye ameachia ngoma mpya ‘Utanipenda’ wiki iliyopita ambayo imekuwa gumzo kwa watu wa kila rika, ana akiba ya hits na collabo za...

Wafanyakazi Wanne wa Serekali Wakiuka Amri ya Rais Magufuli ya Kusafiri Nje ya Nchi Bila Ruhusa ya Rais..Wafukuzwa Kazi

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma. Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa...

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa ...

Rais Magufuli Awahakikishia Watanzania Kutimiza Ahadi Yake Ya Elimu Bure.......Aipongeza TRA kukusanya Trilioni 1.3 Ndani Ya Mwezi Mmoja,Atoa ONYO kwa Wakuu Wa Mikoa

Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300 Kutokana na mafanikio hayo amewahakikishia...

Zitto Kabwe Amtetea Prof Mohongo Kwa Kuchaguliwa Kuwa Waziri, Adai Mwenye Ushahidi Dhidi ya Muhongo Aende Mahakamani

Waliosema Ufisadi ni Mfumo ndio wanasema leo Prof. Muhongo hafai kuwa Waziri sababu ya Tegeta Escrow. Sijui lini mahakama ilimhukumu Muhongo! Sijui lini Muhongo kawa Mfumo. Tujifunze kuweka akiba. Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪TegetaEscrow‬. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka...

Waziri Atoa Mkwara Jeshi la Polisi Atoa Siku Mbili Aletewe Taarifa Kuhusu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Watu Kubambikiwa Kesi

Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo Dec 16 2015 katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi Dar es salaam na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha amepata taarifa kuhusu  udhibiti wa dawa za kulevya. “Wapo wajanja wana mbinu nyingi, lakini hawawezi kutuua. Na mimi hili ni jambo nitalivalia njuga, lakini...

Jumatatu, 14 Desemba 2015

Kazi ya kwanza kuifanya Naibu Waziri Kigwangwala baada ya kuapishwa Dec 12 (+video).

Kwenye zama hizi za Hapa kazi tu za Mheshimiwa Rais John Magufuli,tunashuhudia mambo mengi ambayo mengine tulikua hatuyafikirii kama yanawezekana kufanyika kutoka kwa viongozi wetu,Dec 12 Mawaziri na Manaibu wao walioteuliwa na Rais Magufuli waliapishwa na baada ya kuapishwa...

Giroud na Ramsey waipeleka Arsenal kileleni, huku wakiiombea ushindi Chelsea

December 13 mechi za Ligi Kuu Uingereza ziliendelea kama kawaida, baada ya December 12 kupigwa michezo kadhaa ya muendelezo wa Ligi. Mchezo wa kwanza kupigwa Jumapili ya December 13 wa Ligi Kuu Uingereza ni mchezo kati ya Aston Villa dhidi ya Arsenal. Arsenal wanaoufundishwa na kocha waliyedumu nae kwa...

Real Madrid wakubali kuacha point tatu katika dimba la El Madrigal dhidi ya Villarreal

Baada ya December 12 watani zao wa jadi klabu ya FC Barcelona ya Hispania kucheza mchezo wake wa 15  wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya klabu ya Deportivo La Coruna katika uwanja wao wa nyumbani Nou Camp na kuambulia sare ya kufungana goli 2-2, December 13 ilikuwa zamu ya Real Madrid kucheza dhidi ya Villarreal. Wakati...

Wakati Wapinzani Wakipinga Uteuzi wa Waziri Sospeter Muhongo, Mwenyewe Aibuka na Kusema Haya Makubwa

WAKATI wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka.  Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa...

Wafanyabiashara 15 Waliokaidi Agizo la Rais Kukiona Cha Moto

MAKAMPUNI 15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao, yamejisalimisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini yameshindwa kulipa kodi ndani ya siku saba za msamaha wa Rais John Magufuli. Kodi inayodaiwa kwa kampuni hizo ni Sh bilioni 3.75, hivyo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kukwepa kulipa kodi, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Kaimu...

Mdahalo Wa Tahliso Kujadili Hotuba ya Magufuli Waingia Dosari Baada Ya Wanafunzi wa UDSM Kuupinga

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye  jana alinusuru kuvunjika kwa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO), baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuupinga. Mdahalo huo ulilenga kujadili hotuba ya Rais Dk. John Magufuli aliyosoma bungeni Novemba 20, mwaka huu wakati akizindua Bunge la 11. Dosari ...

Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya  Escrow. Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Handeni, akimnadi...

Asipofunga Zipu…Nay wa Mitego Atakufa Kwa Ngoma

Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’  akijiachia na mrembo mpya mwenye umbo dogo kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar. KIWEMBE! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’ kunaswa akiwa na mrembo mpya mwenye umbo dogo yaani (mbichii) huku...

Nape: Nitaanza Kushughulikia Sheria na Nidhamu Michezoni

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kushughulikia sheria mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo ili kuongeza nidhamu michezoni. Nape aliyeapishwa juzi kuanza kibarua hicho, ataiongoza wizara hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Dk Fenella Mukangara, huku ndoto za Watanzania zikiwa ni kuona kiwango cha michezo kilichoporomoka, kinakua. Akizungumza ...

Diamond Platnumz na Zari Washinda Tuzo Nchini Uganda

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ pamoja na mchumba wake Zarinah Hassan ‘Zari The Bossy Lady’ wamepata Tuzo za Abryanz Style and Fashion (ASFA 2015) zilizofanyika Kampala, Uganda usiku wa kuamkia leo.Wawili hao wameibuka kidedea katika kipengele cha East Africa Most Stylish Couple. Mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda naye ameibuka kidedea...

Jumamosi, 12 Desemba 2015

Yaya Toure ametwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika wa BBC 2015 na kuingia katika rekodi za Okocha na Kanu …

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Toure alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika inayotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Yaya Toure...