Alhamisi, 17 Desemba 2015

Rais Magufuli: Kwa Mara ya Kwanza Serikali Inakusanya Takribani Trilioni 1.3 Kwa Mwezi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amesema kwa mara ya kwanza Serikali itakusanya takribani trilioni 1.3 kwa mwezi.

Pia amewahakikishia watanzania kuwa ahadi yake ya kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ni lazima itekelezwe.

Amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa kodi.

Nyimbo 5 za Diamond zilizopo Store Zitaendelea Kumuweka Kileleni kwa Miaka 10 – Asema Mpiga Picha Wake

Diamond Platnumz ni msanii ambaye (angalau kwa sasa) haoneshi dalili za kushuka kimuziki hivi karibuni. Tunayo mifano mingi ya wasanii wa Bongo ambao waliwahi kufanya vizuri sana na baadaye kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.

Diamond ambaye ameachia ngoma mpya ‘Utanipenda’ wiki iliyopita ambayo imekuwa gumzo kwa watu wa kila rika, ana akiba ya hits na collabo za maana, ambazo kwa mujibu wa mpiga picha wake zinampa uhakika wa kuendelea kukaa kileleni kwa miaka mingine kumi ijayo.

Japo zipo collabo kubwa za kimataifa alizoisha fanya, ameamua kufunga mwaka kwa kuachia wimbo mwingine kabisa ambao hakuna aliyefahamu kama upo wala utafanya vizuri, hii inathibitisha silaha zilizosalia kwenye ‘benki’ yake ya nyimbo huenda yakawa ni mabomu makubwa zaidi.

Collabo zinazosubiriwa kwa hamu ni pamoja na ile ya Diamond na Ne-yo, Diamond na P-Square, Diamond na Usher na zingine.

Wafanyakazi Wanne wa Serekali Wakiuka Amri ya Rais Magufuli ya Kusafiri Nje ya Nchi Bila Ruhusa ya Rais..Wafukuzwa Kazi

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.

Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.

Agizo hilo la Rais Magufuli  lilitolewa jana na Balozi Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa

Rais Magufuli Awahakikishia Watanzania Kutimiza Ahadi Yake Ya Elimu Bure.......Aipongeza TRA kukusanya Trilioni 1.3 Ndani Ya Mwezi Mmoja,Atoa ONYO kwa Wakuu Wa Mikoa

Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300

Kutokana na mafanikio hayo amewahakikishia watanzania kuwa fedha kwa ajili ya kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari ambazo ni kiasi cha shilingi Bilioni 131 zitatengwa mwezi huu na kupelekwa moja kwa moja katika shule husika.

Amesema wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa watapatiwa nakala za taarifa za ugawaji wa fedha hizo na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzitumia vibaya.

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa fedha hizo ambazo ni pamoja na fedha za maendeleo, fedha za mitihani na fedha vifaa vya kufundishia zitaanza kutumwa kila mwezi kuanzia mwezi huu wa kumi na mbili.

Zitto Kabwe Amtetea Prof Mohongo Kwa Kuchaguliwa Kuwa Waziri, Adai Mwenye Ushahidi Dhidi ya Muhongo Aende Mahakamani

Waliosema Ufisadi ni Mfumo ndio wanasema leo Prof. Muhongo hafai kuwa Waziri sababu ya Tegeta Escrow. Sijui lini mahakama ilimhukumu Muhongo! Sijui lini Muhongo kawa Mfumo. Tujifunze kuweka akiba.

Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪TegetaEscrow‬.

Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu.

Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri?

 Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?

Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu.

Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa

1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO

2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania

3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo

By: Zitto Kabwe

Waziri Atoa Mkwara Jeshi la Polisi Atoa Siku Mbili Aletewe Taarifa Kuhusu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Watu Kubambikiwa Kesi

Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo Dec 16 2015 katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi Dar es salaam na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha amepata taarifa kuhusu  udhibiti wa dawa za kulevya.

“Wapo wajanja wana mbinu nyingi, lakini hawawezi kutuua. Na mimi hili ni jambo nitalivalia njuga, lakini kwanini katika ukamataji wa dawa za kulevya sisi tulioko kwenye operesheni tunakaa pembeni? Nataka jibu siku ya Ijumaa”

Kuhusu watu kubambikiziwa kesi, Waziri limemgusa na kalizungumzia pia “Hili la kubambika watu kesi tunaweza kuliondoa hata leo, kikubwa ni kuwa na nidhamu, inakuwaje unambambika mtu kesi ili akuletee pesa? Hiki ni kitendo cha rushwa na tuliangalie kwa pamoja na tutaliongea kwa undani Ijumaa”

Jumatatu, 14 Desemba 2015

Kazi ya kwanza kuifanya Naibu Waziri Kigwangwala baada ya kuapishwa Dec 12 (+video).


Kwenye zama hizi za Hapa kazi tu za Mheshimiwa Rais John Magufuli,tunashuhudia mambo mengi ambayo mengine tulikua hatuyafikirii kama yanawezekana kufanyika kutoka kwa viongozi wetu,Dec 12 Mawaziri na Manaibu wao walioteuliwa na Rais Magufuli waliapishwa na baada ya kuapishwa wapo walioendelea na majukumu yao.
2 
Miongoni mwa Manaibu Waziri walioanza kazi yao mapema ni pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dokta Hamis Kigwangwala baada ya kula kiapo alifanya ziara ya kushtukiza Dec 12 kwenye hospital ya Amana iliyopo Ilala Dar es salaam,nimenasa baadhi ya picha na video mtu wangu.
1 
Hii ni video alipoenda kwenye chumba cha Utra Sound.

Giroud na Ramsey waipeleka Arsenal kileleni, huku wakiiombea ushindi Chelsea


December 13 mechi za Ligi Kuu Uingereza ziliendelea kama kawaida, baada ya December 12 kupigwa michezo kadhaa ya muendelezo wa Ligi. Mchezo wa kwanza kupigwa Jumapili ya December 13 wa Ligi Kuu Uingereza ni mchezo kati ya Aston Villa dhidi ya Arsenal.
3290
Arsenal wanaoufundishwa na kocha waliyedumu nae kwa zaidi ya miaka 12, waliingia katika uwanja wa ugenini wa Villa Park kusaka point tatu dhidi ya wenyeji wao Aston Villa, Arsenal walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, ushindi ambao uliwafanya wavune point tatu na kujikita katika nafasi ya kwanza, huku ikiiombea Chelsea ushindi dhidi ya Leicester City ili iendelee kusalia kileleni.
1330
Kikosi cha Arsenal kiliingia uwanjani kikiwa na nyota wake kama Oliver Giroud aliyefanikiwa kufunga goli la kwanza dakika ya 8 kwa mkwaju wa penati na  Aaron Ramsey aliyefunga goli la pili dakika ya 38 kipindi cha kwanza. Magol ya Arsenal yalidumu kwa dakika zote 90, licha ya Aston Villa kujitahidi kutaka kusawazisha.
1698

Real Madrid wakubali kuacha point tatu katika dimba la El Madrigal dhidi ya Villarreal


Baada ya December 12 watani zao wa jadi klabu ya FC Barcelona ya Hispania kucheza mchezo wake wa 15  wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya klabu ya Deportivo La Coruna katika uwanja wao wa nyumbani Nou Camp na kuambulia sare ya kufungana goli 2-2, December 13 ilikuwa zamu ya Real Madrid kucheza dhidi ya Villarreal.
2F58D34E00000578-3358487-image-a-12_1450040157497
Wakati wapinzani wao wa jadi FC Barcelona wakilazimishwa sare ya goli 2-2 dhidi ya Deportivo La Coruna, Real Madrid imekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Villarreal, Real Madrid walikuwa wanatajwa kuwa na nafasi ya kupunguza point na kuwasogelea wapinzani wao FC Barcelona, Real Madrid walifungwa goli la mapema katika dimba la El Madrigal.
2F58FCC600000578-3358487-image-a-27_1450040779231
Kosa la Luca Modric ndio lilisababisha Roberto Soldado kupewa pasi nzuri na kupachika goli hilo dakika ya 9 ya mchezo, goli ambalo limekuwa gumu kurudi na kuwafanya Real Madrid waondoke vichwa chini katika dimba la El Madrigal. Kwa matokeo hayo, Real Madrid itakuwa imezidiwa point 5 na FC Barcelona wanaoongoza msimamo wa Ligi na yenyewe kubaki nafasi ya 3 katika msimamo wa Ligi.

Wakati Wapinzani Wakipinga Uteuzi wa Waziri Sospeter Muhongo, Mwenyewe Aibuka na Kusema Haya Makubwa


WAKATI wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka. 

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema mbali na mkakati wa kushusha bei ya umeme, kasi ya kusambaza umeme vijijini kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itarejea palepale.
“Nimepokea uteuzi huo, kinachofuata ni kuwatumikia wananchi, niwaombe tu wanivumilie kidogo nitawapa mpango wangu wa maendeleo wa muda mfupi na mrefu, lakini nisisitize tu nishati sio siasa, ni suala la utaalamu, liachwe lifanywe kitaalamu,” alisema Profesa Muhongo.
Akizungumzia bei ya umeme na upatikanaji wake, Profesa Muhongo alisema kupunguza bei hiyo ni ajenda muhimu itakayozingatiwa na kusema ili umeme uwe wa uhakika, ni lazima kuwe na mipango ya kuwa na nishati hiyo ya uhakika ifikapo mwaka 2025.
“Umeme wa uhakika utapatikana na matarajio yetu ni Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo tunatarajia uzalishaji wa nishati hiyo ufike Megawati 10,000 hadi 15,000,”alisema Profesa Muhongo.
Alisisitiza kwamba wizara yake haitategemea chanzo kimoja cha nishati bali wataangalia vyanzo vingine ikiwemo nishati jadidifu, upepo, gesi, makaa ya mawe, maji huku akisema vyanzo hivyo vikitumika kuzalisha nishati, ni wazi bei ya umeme itashuka na kushusha gharama nyingine za maisha na za uwekezaji.
Aliongeza katika kuendeleza sekta ya nishati suala la uwekezaji ni muhimu hivyo wizara yake inakaribisha wawekezaji wenye sifa, watakaowekeza kwenye sekta hiyo ili kuja na matokeo bora zaidi, wananchi wanufaike na rasilimali za nchi yao.
Pamoja na nia yake hiyo kwa wananchi, Profesa Muhongo anakabiliwa na pingamizi kutoka kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani, akiwemo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Lissu na Profesa Lipumba, wamekaririwa wakikosoa uteuzi wa Profesa Muhongo kwa madai kuwa wizara aliyopewa kuiongoza, ilikumbwa na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow wakati wa uongozi wake, ikasababisha ajiuzulu.
Hata hivyo, Profesa Lipumba na Lissu katika kukosoa huko, hawakutaka kutumia kumbukumbu zilizo wazi kuwa uchunguzi dhidi ya Profesa Muhongo, ulibaini kuwa hakukiuka maadili yoyote katika sakata la utoaji wa karibu Sh bilioni 300 zilizokuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT).
Matokeo ya uchunguzi huo yalitangazwa Mei mwaka huu na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ambapo alisema Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ndiyo ilifanya uchunguzi kama Profesa Muhongo alistahili kwenda kwenye Baraza la Maadili kujibu mashitaka, lakini hawakuona tatizo lake na kufunga shauri lake.
Balozi Sefue aliweka wazi kuwa Profesa Muhongo alijiuzulu kwa sababu za kisiasa, lakini kimaadili hakuhusika kwa namna yoyote, kutokana na uchunguzi wa Sekretarieti ndiyo sababu hakufikishwa katika Baraza la Maadili.
Kitu kingine ambacho Lissu na Profesa Lipumba, hawakutaka kuzungumzia ni utendaji wa Profesa Muhongo alipokuwa katika wizara wakati wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Kumbukumbu zinaonesha kuwa katika miaka miwili ya uongozi wake katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Muhongo alisimamia kwa umahiri usambazaji wa umeme vijijini. 

Kabla ya kuteuliwa kwa Profesa Muhongo, Watanzania asilimia 14 tu ndio waliokuwa wakitumia nishati ya umeme, kati yao asilimia 12 walikuwa watumiaji wa mijini na asilimia mbili ndio walikuwa watumiaji wa vijijini.
Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, kati ya mwaka 2007 na mwaka 2010, kulikuwa na ongezeko la asilimia nne la watumiaji wa umeme, hali iliyoonesha kuwa ongezeko la Watanzania waliokuwa wakipata umeme, lilikuwa asilimia moja kwa mwaka. 

Lakini baada ya kuteuliwa kwa Profesa Muhongo katika nafasi hiyo, katika muda mfupi wa uongozi wake, idadi ya Watanzania wanaotumia umeme iliongezeka na kufikia asilimia 36 katikati ya mwaka jana.
Kwa hatua hiyo, uongozi wa Profesa Muhongo ulivuka malengo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo ndio msingi wa utekelezaji wa malengo ya Serikali, iliyotaka Serikali kuhakikisha ifikapo mwaka 2015, asilimia 30 ya Watanzania wawe wanapata umeme.
 Katika kutimiza malengo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010, uongozi wa Profesa Muhongo, ulitangaza punguzo la gharama za kuunganisha umeme majumbani kutoka Sh 177,000 za awali hadi Sh 27,000 vijijini.
Awali, punguzo hilo lilitolewa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara, ambako bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam limeanzia na limepita, lakini baada ya muda gharama hizo zilishushwa kwa vijiji vyote nchi nzima.
Profesa Muhongo mwenyewe alikaririwa akisema gharama hizo zitahusu miradi inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), katika kipindi ambacho makandarasi watakuwa wakiendelea na awamu ya pili ya miradi iliyoanza Machi mwaka huu na kutarajiwa kukamilika katikati ya mwakani.

Wafanyabiashara 15 Waliokaidi Agizo la Rais Kukiona Cha Moto


MAKAMPUNI 15 yaliyokwepa kodi baada ya kutorosha makontena yao, yamejisalimisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini yameshindwa kulipa kodi ndani ya siku saba za msamaha wa Rais John Magufuli.
Kodi inayodaiwa kwa kampuni hizo ni Sh bilioni 3.75, hivyo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kukwepa kulipa kodi, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Philip Mpango alisema hayo jana wakati akielezea makusanyo ya kodi ya makontena yaliyoondolewa katika bandari kavu ya Azam, kinyume cha sheria pamoja na kumalizika kwa siku saba alizotoa Rais Magufuli kwa wafanyabiashara hao kulipa kodi waliyokwepa, bila kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
Dk Mpango alisema siku hizo saba zimefikia kikomo juzi, hivyo hatua kali za kisheria kwa wafanyabiashara ambao hawakulipa kodi katika kipindi hicho zinafuata hivyo wasubiri cha moto.
“Tumewasihi waje kulipa kwani huruma ya Rais sasa imeisha... tulifanya uhakiki na kuthibitisha kuwa kampuni hizo zipo. Wamekuja kulalamika lakini hakika hakuna atakayesamehewa kulipa na sasa tunafuata mkondo wa sheria ili kuwafikisha mahakamani,” alisisitiza.
Wadaiwa 
Alitaja kampuni hizo kuwa ni Ahmed Saleh Tawred anayedaiwa Sh milioni 59.23; Cla Tokyo Limited Sh milioni 77.52; Farida Abdullah Salem Sh milioni 75.33 na Juma Kassem Abdul Sh milioni 190.18.
Wengine ni Libas Fashion Sh milioni 52.94; Rushy Wheel Tyre Center Co Ltd, Sh bilioni 1.8; Said Ahmad Hamdan Sh milioni 68.36; Said Ahmed Said Sh milioni 68.73 na Salum Continental Co Ltd Sh milioni 151.17.

 Pia yumo Salum Link Tyres Sh milioni 343.44; Simbo Yonah Kimaro, Sh milioni 69.22; Snow Leopard Building Material Co Ltd Sh milioni 93.97; Swaleh Mohamed Swaleh Sh milioni 34.68; Tybat Trading Co Limited, Sh milioni 598.69 na Nasir Saleh Mazrui Sh milioni 70.10.
Alisema mpaka kufikia jana TRA walikuwa wamekusanya Sh bilioni 10,643.004,948.46 kutoka kwa kampuni 28 ambapo kampuni 13 zimelipa kodi yote iliyokadiriwa, ambayo ni Sh 4,167,130,173.89 na Sh 2,303,637,554.57 kutoka kampuni 15 zilizolipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa.
Dk Mpango alisema Sh bilioni 4.17 zimelipwa na kampuni ya Azam ICD, ikiwa ni dhamana ya kodi iliyokwepwa, hivyo atatakiwa kumaliza kulipa kodi yote inayodaiwa kwa mujibu wa nafasi yake kama mwenye dhamana.
Alisema wakati utekelezaji huo ukiendelea, ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi hiyo ya makontena yaliyoondolewa bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha, TRA imefungua akaunti maalumu katika Benki Kuu yenye namba 9921169785 inayoitwa Commissioner for Customs and Excise – Container Account.
Kwa mujibu wa Dk Mpango, mpaka sasa watumishi 36 wa TRA wanaotuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na makontena hayo kuondoshwa bandarini.
Watumishi wachongewa 
Aidha, alisema TRA imepata taarifa zisizopungua 15 kutoka kwa wananchi kuhusu mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi na walipakodi wanaokwepa kodi. 

Aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa na kuwaomba wengine wajitokeze kutoa taarifa zaidi na mamlaka hiyo inawahakikishia kuwa itawalinda.
Dk Mpango alisema wanaendelea kutekeleza maagizo ya Rais katika ukusanyaji wa mapato, ikiwa ni pamoja na kupiga picha makontena yote badala ya sampuli ya kontena ilivyo sasa na wanafanya utaratibu wa kupata mashine za kupiga picha za nyongeza.

Mdahalo Wa Tahliso Kujadili Hotuba ya Magufuli Waingia Dosari Baada Ya Wanafunzi wa UDSM Kuupinga

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye  jana alinusuru kuvunjika kwa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO), baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuupinga.

Mdahalo huo ulilenga kujadili hotuba ya Rais Dk. John Magufuli aliyosoma bungeni Novemba 20, mwaka huu wakati akizindua Bunge la 11.

Dosari hiyo ilijitokeza mapema kabla ya Nape kuwasili katika ukumbi wa Nkurumah baadaya Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), Kataponda Ahadi kusimama na kutoa hoja ya kuwataka wenzake wasusie mdahalo huo kwa sababu haukubeba ajenda na lengo la TAHLISO.

Hata hivyo, alikatishwa mazungumzo yake baada ya kuelezwa muda wa kujadili mada ulikuwa haujaanza, kwa sababu wakati huo  mdhamini wa mdahalo huo ambao ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alikuwa akielezea faida za mfuko huo.

Baada ya malumbano yaliyochukua muda kidogo, wanafunzi hao walikubaliana na hoja ya  kuendelea kumsikiliza mwakailishi wa NSSF aliyekuwa akiwasilisha mada, hadi Nape alipowasili ukumbini hapo.



Katika hotuba yake, Nape aliusifia mdahalo huo na kusema utasaidia wabunge watakapo kwenda bungeni wawe na ajenda za wananchi, badala ya kwenda na ajenda zao ambazo pengine si matatizo wanayopata wananchi.

Alisema hotuba ya rais, imekuja kwa wakati na imeeleza changamoto nyingi, hivyo ni muhimu vijana wakawa sehemu ya mabadiliko yanayotakiwa kwa staha na uwazi.

Aliwataka wananchi waache utaratibu wa kusikiza na kushangilia tu, bali waichambue, waikosoe,washauri na kuwasisitiza kuwa wasiache suala la mabadiliko liwe la Rais Dk. Magufuli tu.

“Lazima tuhakikishe mabadiliko haya yanaingia kwenye mfumo na yasibaki kwa rais peke yake ili siku tukimpata mtu mwingine afuate mfumo huo. Inapaswa tuusukume mfumo ukubali  mabadiliko hayo lakini mfumo ukigoma tutapata matatizo,” alisema Nape.

Baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wanafunzi walinyoosha mikono kutaka kutoa hoja ambapo mshereheshaji aliwataka wasubiri mada zitakapowasilizwa wahusika ndiyo wapate muda wa kuzijadili.

Hata hivyo, wanafunzi hao hawakukubaliana na mwongozo huo na walisimama na kusema wana hoja ya kumweleza waziri kabla mada hazijawasilishwa na ndipo mmoja alipopewa nafasi.

Mwanafunzi huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake, alisimama na kuanza kutupa lawama kwa TAHLISO kuwa wameshindwa kusikiliza na kujadili matatizo yanayowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu na badala yake wanajihusisha na mijadala ya kisiasa.

“Tunashangaa TAHLISO ambayo ni shirikisho la kuwatetea wanafunzi wa vyuo vikuu, wamekaa kimya kila tunapofikisha matatizo ya wanafunzi, sasa wameona bora wajadili hotuba ya Dk.Magufuli,” alisema mwanafunzi huyo ambaye kabla hata hajamaliza kutoa hoja yake aliamriwa kuketi.

Kitendo hicho kiliamsha hisia kwa wanafunzi wengine, ambao walisimama na kuanza kupaza sauti wakipinga mdahalo huo kwa madai kuwa hauna maslahi ya wanafunzi na kwamba ni wa kisiasa.

Hali hiyo ilimlazimu mshereheshaji kuwaomba askari kuingia ndani ili kuwatoa wanafunzi hao ambao hata hivyo waliamua kutoka wenyewe wakiongozwa na rais wao huku wakiendelea kuituhumu jumuiya hiyo.

Walipofika nje ya ukumbi waliendelea kupiga kelele ambapo iliwalazimu baadhi ya viongozi wa TAHLISO kutoka nje na kuwataka waondoke katika eneo hilo.

Yaliibuka mabishano baina ya viongozi wa pande hizo mbili na baadhi ya wanafunzi ambapo Waziri Nape aliamua kutoka nje na kuacha mdahalo ukiendelea na alipofika nje aliomba kusikiliza hoja zao.

Akielezea malalamiko yao, Rais wa DARUSO Ahadi alisema TAHLISO imeshindwa kusimamia maslahi ya wanafunzi hasa pale wanapoomba kukutana ili kujadili masuala ya wanafunzi wamekuwa hawajitokezi.

“Hawa kwenye mambo yanayohusu wanafunzi wanakaa kimya, mdahalo wameweza kuandaa kujadili hotuba ya Rais Magufuli, zaidi hata huu mdahalo unaofanyika hapa kwetu sisi viongozi wa DARUSO ambao pia ni wajumbe wake hatujapewa taarifa, ndio maana tumeamua kuupinga,” alisema Ahadi.

Kwa upande wake, Waziri wa Mikopo wa DARUSO, Shitindio Venance, alisema: “Kutokana na kitendo cha jumuiya hii kushindwa kutatua matatizo yetu tumeamua kuunda Kamati ya Taifa ya kufuatilia Mikopo ya wanafunzi nchi nzima na hivi tunapozungumza hapa kuna wanafunzi wapatao 80 ambao wanatakiwa wafungashe warudi nyumbani kwa kukosa mikopo na wengine wapo Chuo cha Bagamoyo lakini tunashangaa TAHLISO ipo kimya,”alisema.

Naye Makamu wa Rais wa DARUSO, Irene Ishengoma, alimweleza Nape kuwa pamoja na kusumbuliwa kwa kunyimwa mikopo, bado Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekuwa ikiwatoza sh 20,000 za kuiendesha suala ambalo ilitakiwa yenyewe itafute mbinu za kujiendesha.

Akijibu hoja hizo Nape aliwataka viongozi hao kuitisha vikao ili kuwaondoa viongozi wa TAHLISO ambao wameonekana kushindwa kazi kwani wao ndio waliowaweka na hivyo wana mamlaka ya kuwaondoa.

“Unajua tatizo lenu ni dogo…hawa viongozi mmewaweka wenyewe na kwa kawaida mwiba unapoingilia ndipo unapotokea hivyo nyie ndio wakuwatoa, tumbueni majipu kama mnaona yapo,” alisema Nape.

Kuhusu matatizo ya mkopo, Nape aliwaambia tayari yanajulikana na kwamba licha ya kwamba yeye si waziri mwenye dhamana lakini ni kiongozi wa chama kilichopo madarakani hivyo atahakikisha leo watahakikisha, tatizo hilo linakoma.

“Naomba niwahakikishie kuwa ikifika kesho (leo) wanaohusika tutakwenda kuwashughulikia ili wakawajibike kwa sababu inaonekana kuna tatizo maana wanafunzi wakigoma fedha zipo lakini wakikaa kimya hawapewi,” alisea Nape.

Nape alifanikiwa kumaliza dosari hiyo iliyodumu kwa dakika 20 baada ya kuwaomba wanafunzi hao warudi ukumbini ili kuendelea na mdahalo kwasababu kama ni matatizo yao yamefika sehemu husika ambapo walikubali na kurudi ukumbini.

Ndani ya ukumbi huo mada zilikuwa zinaendelea ambapo akichambua hotuba ya Rais Magufuli, Mtaalamu wa Mambo ya Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk. Honest Ngowi alisema kiuchumi suala la elimu bure halipo kwani elimu hiyo inalipiwa kwa ruzuku ya serikali kwa asilimia 100.

Alisema ili kuweza kutekeleza hilo wananchi wanatakiwa kukubali kulipa kodi zilizowekwa kwasababu ndizo zitakazotumika kuendesha sekta hiyo.

Naye Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa (UDSM), Dk. John Jingu alisema hotuba hiyo ilijikita katika dira ya maendeleo ya Taifa ifikapo mwaka 2025 ya kuwa na uchumi wa kati, kwani rais ameweza kuonesha njia na nia ya kutekeleza dira hiyo.
Kwa upande wake Mwanadiplomasia mkongwe, Balozi Christopher Liundi alisema hotuba ya Rais Magufuli imekuwa mfano kwa viongozi wa chini yake, kwani wanaonekana kutenda kwa kasi yake tangu aingie madarakani.

Chadema Bado Hawajakubali Yaishe...Waapa Kumshughulikia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo Bungeni

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahidi kumshughulikia Bungeni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kikidai kuwa bado hajasafishwa kwenye kashfa ya akaunti ya  Escrow.

Ahadi hiyo ilitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Handeni, akimnadi Daudi Lusewa.

Alisema baadhi ya mawaziri, akiwamo Muhongo, bado hawajasafishwa na tuhuma za rushwa zilizosababisha wajiuzulu hivyo wajiandae kwani wabunge wa chama hicho wamejiandaa kumwangusha.

Mnyika alisema amemshangaa kuona Rais John Magufuli akimteua Muhongo kwenye Wizara ile ile alikopatia kashfa, iliyosababisha Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtema kwenye Baraza la Mawaziri.

“Hatukubaliani na uteuzi wa Profesa Muhongo na namhakikishia bungeni patachimbika,” alisema Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba, Dar es salaam.

“Hoja yetu ya kwanza tutakapoingia bungeni tu itakuwa kushinikiza Waziri huyu ajiuzulu maana bado hajasafishwa,” alisema Mnyika.

Asipofunga Zipu…Nay wa Mitego Atakufa Kwa Ngoma

NAY (2)Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’  akijiachia na mrembo mpya mwenye umbo dogo kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.

KIWEMBE! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’ kunaswa akiwa na mrembo mpya mwenye umbo dogo yaani (mbichii) huku rekodi ikionesha ndani ya muda mfupi ameshabadilisha warembo takriban wanne hali ambayo imesababisha wadau kumpa tahadhari kwamba asipofunga zipu, ataukwaa Ukimwi a.k.a Ngoma, Risasi Jumamosi lina mchongo kamili.
NAY (3) 
TUKIO JIPYA
Achana na Siwema Edson, Shamsa Ford, Stella Tilya ‘Chaga Baby’ aliowapitia katika kipindi kifupi, mapema wiki hii Nay amenaswa na mrembo mbichii aliyefahamika kwa jina la Ana wakifanya yao kwenye bwawa la kuogelea katika Hoteli ya White Sands iliyopo Mbezi Beach jijini Dar.
NAY (4)Nay wa Mitego akifanya yake.
ENEO LA TUKIO
Awali, Mbongo Fleva huyo alionekana akiwa ameketi pembezoni mwa Bahari ya Hindi na baada ya saa moja mbele alielekea kwenye bwawa na kuanza kuongelea akiwa ameambana na mrembo huyo.
NEY-1Siwema akiwa na Nay enzi wakiwa wapenzi.

“Amefika (Nay) na vijana kama wanne hivi na huyo mrembo alikuwa wa tano, mwanzo wakati wakija yule mrembo alikuwa karibu na jamaa mmoja bonge sijui ndiye meneja wake wa sasa, kwa hiyo muda wote nilihisi huyo demu ni wa Bonge kumbe ilikuwa zuga tu maana baada ya kuanza kuogelea demu akaonesha wazi kuwa ni mali ya Nay kwani alikuwa anamfanyia kila linalostahili mtu na mpenzi wake kufanyiana,

AONYWA KUHUSU NGOMA
“Halafu huyu jamaa atakufa kwa ngoma asipokuwa makini maana anabadili warembo kama kitu gani.
Msururu wake unamweka pabaya. Kuna warembo wengi sana kawapitia, maarufu na wasio maarufu. Juzikati alikuwa na Siwema, mara Shamsa, ghafla nikasikia yupo na Chaga Baby leo tena ana kifaa kipya, asipofunga zipu ngoma inamuiita,” alinyetisha mdaku mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.
Chaga Baby akiwa katika pozi.

‘KANGAA FOTO’
Kama vile staa wa dansi kutoka Kongo, Koffi Olomide anavyoimba katika wimbo wake wa Selfie, ndivyo paparazi wetu alivyoanza kumtandika picha za kutosha Nay na mrembo huyo walipokuwa wakioga kwa kushikana shikana maeneo ‘muhimu’ ambapo wote kwa pamoja walionekana kufurahi.

WALA PIZZA
Kama hiyo haitoshi, wawili hao baada ya kujiachia katika bwawa hilo kwa zaidi ya saa mbili, walitoka na kuagiza msosi unaojulikana kwa jina la ‘pizza’ ambapo pia walikula kwa staili ya mtu na bebi wake bila kuhofia macho ya watu.
IMG_0093Nay wa Mitego akiwa na Shamsa Ford.

NAY ABANWA, ACHEKA
Baada ya paparazi wetu kukusanya ushahidi wa kutosha juu ya matukio yake ya kimahaba ndani ya maji, alimbana Nay ambaye alishindwa kutoa majibu yaliyonyooka kama kweli aliyekuwa naye ni kifaa chake kipya ama laa!

“Dah, wewe umefikaje hapa na umenionaje? Au kuna mtu kakulengesha nini kwangu, maana si rahisi mwandishi kama wewe kuja hivihivi tu hapa! Si bure utakuwa umepewa umbeya huu na mtu.
ney_wa_mitego_nishaNisha akiwa na Nay.
Risasi Jumamosi: Sasa huyu ndiye mpya au unawachanganya pamoja na yule wa Marekani, Chaga Baby?

Nay: Ebwana huyu anaitwa Ana ni mtu wangu tu, nipo na masela zangu wengine, tumekuja kuogelea kwa raha zetu so haya ni maisha fulani ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo na kujiachia kwani kuna tatizo?
Risasi Jumamosi: Hauogopi Ukimwi kujiachia na warembo tofauti?

Nay: Kwani nimekwambia huyu ni mtu wangu? Mimi niko makini kweli na suala la ngoma. Naomba uniache niondoke naona unaniharibia siku.

MSURURU WA NAY
Ukiondoa Siwema, Shamsa, Chaga Baby huko nyuma jamaa huyo kwa nyakati tofauti alishawahi kuripotiwa kubanjuka na mastaa wa Bongo Movies; Salma Jabu ‘Nisha’ na Skyner Ally ‘Skaina’ aliyezaa naye mtoto mmoja.


Nape: Nitaanza Kushughulikia Sheria na Nidhamu Michezoni

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ameahidi kushughulikia sheria mbalimbali zinazosimamia sekta hiyo ili kuongeza nidhamu michezoni.

Nape aliyeapishwa juzi kuanza kibarua hicho, ataiongoza wizara hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Dk Fenella Mukangara, huku ndoto za Watanzania zikiwa ni kuona kiwango cha michezo kilichoporomoka, kinakua.

Akizungumza na mwandishi wetu jana alisema utovu wa nidhamu kwa baadhi ya viongozi na wachezaji umekuwa ukiitafuna sekta hiyo kwa kiwango kikubwa na kusababisha kushuka kwa michezo.

Alisema zipo baadhi ya sheria zinazohitaji marekebisho ili ziwe na tija na kwamba ana uhakika kuwa zitasaidia kurejesha thamani ya michezo, ikiwamo soka na sanaa.

“Michezo ikisonga mbele na timu zetu zikifanya vizuri tutavutia wawekezaji wengi kwenye sekta hii kwa sababu suala siyo kufurahi, tunatakiwa tuichukulie sekta hii muhimu kama sehemu ya kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa Taifa letu na mtu binafsi,” alisema Nnauye na kuongeza:

“Ni kweli kwamba kiwango cha michezo nchini kipo chini na maeneo ya mwanzo ya ninayodhani yanapaswa kushughulikiwa ni kwenye sheria. Natamani kuona tunakuwa na sheria zenye tija, zitakazosaidia kumaliza utovu wa nidhamu unaoitafuna sekta hii,” alisema.

Diamond Platnumz na Zari Washinda Tuzo Nchini Uganda

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ pamoja na mchumba wake Zarinah Hassan ‘Zari The Bossy Lady’ wamepata Tuzo za Abryanz Style and Fashion (ASFA 2015) zilizofanyika Kampala, Uganda usiku wa kuamkia leo.Wawili hao wameibuka kidedea katika kipengele cha East Africa Most Stylish Couple.

Mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda naye ameibuka kidedea katika tuzo hizo kwa kipengele cha Mbunifu Bora wa Mwaka huku Mwanamitindo Bora wa Mwaka ikienda kwa Mtanzania mwingine, Dax Hannz.

Mbali na hao, pia Tanzania imepata tuzo kupitia staa wa kike wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee aliyepata katika kipengele cha East Africa’s best Dressed Female Artist.
Katika sherehe hizo zilifunikwa kwa shoo kutoka kwa mkali kutoka Nigeria, Banky W akishirikiana na bidada kunako Bongo Fleva, Linah.

Jumamosi, 12 Desemba 2015

Yaya Toure ametwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika wa BBC 2015 na kuingia katika rekodi za Okocha na Kanu …



Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Toure alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika inayotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Yaya Toure amefanikiwa kuibuka na ushindii wa baada ya kupata kura nyingi zaidi ya Pierre-Emerick AubameyangAndre AyewYacine Brahimi na Sadio Mane.
86610826_afoty-2015
List ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa BBC
Kutwaa tuzo hiyo kwa Yaya Toure kunamfanya kuwa mchezaji wa tatu kuingia katika rekodi ya wachezaji wa zamani wa Nigeria Nwankwo Kanu na Jay-Jay Okocha ambaoo kila mmoja katwaa tuzo hiyo mara mbili, rekodi ambayo inashikiliwa na wachezaji watatu kwa sasa ikiwemo Toure.
e
List ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo hiyo
Toure kwa mara ya kwanza alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC mwaka 2013, baada ya ushindi wa tuzo hiyo hii ni moja kati ya sentensi za Yaya Toure “Najivunia kupokea tuzo hii kutoka kwa mashabiki wangu siwezi kuamini”