Jumanne, 9 Desemba 2014

Umeipata hii ya Daktari feki aliyekamatwa Taasisi ya MOI?

Hosp
Moja kati ya matukio yaliyochukua headline ni hili tukio la kukamatwa Daktari feki, Dismas Macha katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) akiwa amevaa sare za kazi kama Daktari ambapo hii inakuwa mara ya pili kukamatwa akiwa anachangisha rambirambi kwa Madaktari akidai kuwa amefiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo ya MOI, Dk Othman Wanin Kiloloma amesema; “Tumekuwa tuna tatizo kubwa la kuletewa watu wanaokuja wao na kujitia ni madaktari wakiomba watu pesa, wakiomba waweze kupewa takrima na hata michango mingine na wamefikia hatua sasa ya kuwatapeli hata madaktari wenyewe kwa kuomba michango na vitu vingine
Leo tumewaita Waandishi wa Habari kuwaeleza kisa cha mtu ambee amekuja na kujitia yeye ni Daktari wa sehemu ya taasisi na anaomba michango mbalimbali, na mtu huyu sii mara ya kwanza amekuwa akishikwa Muhimbili sehemu tofauti kwa wakati tofauti kwa hiyo tumewaita ili muweze kumtambulisha kwa jamii asiweze kudanganya watu wengine kwamba yeye ni Daktari”– Dk. Kiloloma.
Mwananchi mmoja ambaye alikuwa mmoja ya watu walishuhudia mtu huyo kukamatwa amesema; “Suala la Madaktari feki tatizo kubwa lililopo sio Madaktari feki kama hivyo kuna Mahakimu feki, Madaktari feki, ukishaona mahali popote anatokea mtu feki ujue kuna maslahi na tatizo kubwa linalojitokeza kwenye Hospitali ni ukifika Madaktari wenyewe halisi wanataka fedha ili wakuhudumie, kwa hiyo yoyote anaweza kujifanya feki kwa maana anakusanya fedha za Watanzania alafu anatoweka kwa hiyo anakuwa amekula fedha…

Jumatatu, 8 Desemba 2014

DADA WA KAZI ALIYEMTESA MTOTO UGANDA AOMBA MSAMAHA

Jolly Tumuhirwe
Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.
Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
 Jolly Tumuhirwe ameomba mahakama kumsamehe kwa kumtesa mtoto 

Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.
Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.
Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mianne au adhabu zote mbili.

Nguvu ya Mapenzi itamrudisha Chris Brown kwa Karrueche? Soma alichokiandika @Instagram

chris-brown-and-karrueche
Weekend iliyopita imeisha kwa habari za kuisha kwa penzi la Chris Brown na Karrueche, halafu story kuibwa ya pili ikawa yale madongo ambayo kila mmoja akimtuhumu mwenzake kwamba  ndiye sababu ya mapenzi yao kuisha.
Imekuwa ni kama mchezo wa kuigiza kwa wawili hao kuachana na kurudiana, lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram Chris ameandika ujumbe wa kumuomba radhi Karrueche huku akisema hajali watu wanamchukuliaje.
Ujumbe huo unasomeka hivi;Being young and dumb is one of my strong suits and emotional at best. I love hard and react impulsively when I’m hurt at times. I don’t think social media is a place to air out or hash out personal problems and a nigga feel hella WACK for doing it. So I AM APOLOGIZING I live in a glass house and the same sh*t that makes me great also is my curse. Everybody know I love that girl. I don’t care how my image my look to the public because I’m still gonna be the best at what I do. I just want baby girl to know I apologize!
Ujumbe huo umewekwa na picha hii
Karu & cHRIS

TAKWIMU MBAYA KWA ARSENAL.

wenger
Hali ndani ya klabu ya Arsenal imezidi kuwa mbaya baada ya mashabikiw a klabu hiyo kuendelea kushinikiza kuondoka kwa kocha wao Arsene Wenger . Shinikizo hilo liliongezeka mwishoni wa wiki iliyopita wakati Arsenal ilipofungwa na Stoke City kwa matokeo ya 3-2 kwenye uwanja wa Brittania .
Mashabiki wa Arsenal baada ya mchezo huo walichapana Makonde baada ya kutokea mabishano makubwa baina ya makundi mawili ambayo mojawapo lilikuwa linaunga mkono Wenger Kuondoka huku lingine likimtaka kocha huyo aendelee kubaki madarakani.
Wachezaji wa Arsenal wakionesha masikitiko baada ya kufungwa moja kati ya mabao matatu waliyofungwa na Stoke City.
Wachezaji wa Arsenal wakionesha masikitiko baada ya kufungwa moja kati ya mabao matatu waliyofungwa na Stoke City.

Takwimu zinazidi kuwapa sauti wale wanaotaka Wenger aondoke ambapo imefahamika kuwa Arsenal imekuwa ikifungwa baada ya wapinzani wake kupiga shuti la kwanza lililolenga shabaha ya lango katika michezo takribani saba kati ya 15 ambayo Arsenal imecheza. Hadi sasa Arsenal ambayo iko kwenye nafasi ya tano ambaimekusanya pointi 23 baada ya michezo 15 huku ikiwa imeshinda michezo 6 pekee , ikitoka sare kwenye michezo mitano na kupoteza michezo sita .
Arsenal imefungwa mabao saba yaliyotokana na shuti la kwanza katika michezo saba kati ya 15 ya ligi ya England.
Arsenal imefungwa mabao saba yaliyotokana na shuti la kwanza katika michezo saba kati ya 15 ya ligi ya England.
Mabingwa hawa wa kombe la FA wataingia uwanjani hapo kesho kutafuta tiketi ya kufuzu hatua ya 16 kama washindi wa kundi lake watakapokuwa wanacheza na Galatasaray ya Uturuki.

Jumapili, 7 Desemba 2014

Kiongozi wa Al-Qaeda auawa Pakistan

 
Kiongozi wa Oparesheni wa kundi la Al Qaeda auawa nchini Pakistan katika uvamizi. 


Kiongozi mwandamizi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda anayeshukiwa kupanga kulipuwa treni mijini New York na London ameuawa nchini Pakistan,kwa mujibu wa Jeshi la nchi hiyo.
Adnan el Shukrijumah aliuawa katika shambulizi kazkazini magharibi mwa Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan,jeshi hilo limesema.
Maafisa wa kundi la Ujasusi kutoka Marekani FBI wamekuwa wakimtaja kuwa mkuu wa kitengo cha oparesheni katika kundi la Al Qaeda,wadhfa ambao ulishikiliwa na mtu anayeshukiwa kupanga njama za shambulizi la Septemba 11 Khalid Sheikh Mohammed.
Shukrijumah alizaliwa nchini Saudi Arabia na kuishi kwa miaka kadhaa nchini Marekani.
Aliorodheshwa katika mashtaka kama muhusika wa kupanga njama katika kesi dhidi ya watu watatu wanaoshutumiwa kwa kupanga mashambulizi ya kujitolea muhanga katika barabara za treni mjini New York mwaka 2009.
Pia anashukiwa kupanga njama za kutekeleza mashambulizi ya kundi ya Al Qaeda nchini Panama,Norway na Uingereza.
Uvamizi huo wa mapema leo ulifanyika katika jimbo la Shinwarsak kusini mwa Waziristan,ambalo ni eneo la Kazkazini magharibi mwa mkoa uliopo karibu na mpaka.
Jimbo hilo ni kambi ya wapiganaji wa Taliban nchini Pakistan na washirika wao.

Taarifa nyingine kutoka Ikulu kuhusu Rais Kikwete leo Desemba 07

20060301195016!Dar_Ikulu-tz 
Tulisikia kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji Marekani, Rais Kikwete alipewa masharti kadhaa na madaktari waliomfanyia upasuaji juu ya utaratibu wa kufanya katika kipindi cha miezi mitatu, ambapo moja ya masharti aliyopewa ni kutofanya kazi ngumu.
Katika ukurasa wa Facebook wa gazeti la Mwananchi, wamepost picha na story inayosomeka hivi; “..MAZOEZI: Rais Jakaya Kikwete akifanya mazoezi katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, kutekeleza ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara tatu kwa siku ili kuimarisha afya yake, baada ya upasuaji mwezi uliopita nchini Marekani. Picha na Ikulu..
10426665_10152868806749339_9162170230645207565_n

Jumamosi, 6 Desemba 2014

Rapper mwingine wa TZ aliyetunukiwa shahada ya kwanza chuo kikuu

.
.
Rapper kutokea Unity Entertainment Stereo ambaye ameachia wimbo wake uitwao ‘Wako’ aliomshirikisha muimbaji wa Kenya,Victoria Kimani leo Des 6  ameongezewa CV yake ya Elimu baada ya kutunukiwa shahada ya ‘Bachelor of Science in Urban and Regional Planning’  kutoka chuo kikuu cha Ardhi Dar es Salaam.

EPL: Mambo yazidi kuwa magumu kwa Wenger: Matokeo ya Stoke vs Arsenal

IMG_9342.JPG
Wakati akiwa kwenye shinikizo la kutakiwa kutimuliwa, mambo yamezidi kuwa magumu kwa kocha mkongwe zaidi kwenye ligi kuu ya England Arsene Wenger.
Akiiongoza timu kwenda mpaka kwenye dimba la Brittania kucheza dhidi ya Stoke City, na kilichotokea ni majonzi zaidi kwa mashabiki wa Gunners.
Mpaka kufikia mapumziko Arsenal walikuwa nyuma kwa jumla ya magoli 3 kwa nunge.
Magoli ya Peter Crouch, Jonathan Walters na Bojan Kirkic yaliipa Stoke uongozi kwenye mchezo huo.
Kipindi cha pili Bojan aliichambua ngome ya Arsenal na kufunga goli zuri kabla ya mwamuzi wa pembeni kuamua ni offside- na dakika moja baadae Arsenal wakapata penati iliyofungwa na Santi Cazorla.
Dakika baadae Gunners wakafunga goli la pili kupitia Aaron Ramsey.
Wakiwa wanatafuta goli la kusawazisha beki Chambers akapata kadi nyekundu lakini hiyo haikupunguza kasi ya Arsenal kutafuta goli, lakini mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho matokeo ya Stoke 3-2 Arsenal.

Ijumaa, 5 Desemba 2014

MKUU WA USALAMA WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHINA AKAMATWA

 
Aliyekuwa mkuu wa usalama nchini China Zhou Yongkang amefukuzwa kutoka Chama cha Kikomunisti na atafunguliwa mashtaka huku kukifanyika uchunguzi wa ufisadi. Zhou alikuwa kiongozi wa kitengo cha usalama cha China kabla ya kustaafu miaka miwili iliyopita na atakuwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa chamani kutuhumiwa kwa madai ya ufisadi na kufunguliwa mashtaka. Uamuzi wa kumkamata na kumtimua afisa huyo mkuu wa Kamati kuu ya chama cha Kikomunisti yenye wanachama 9 ulifikiwa katika mkutano wa baraza kuu la chama hicho lenye wanachama 25 hapo jana, kufuatia uchunguzi rasmi uliofanyika mapema mwaka huu. Zhou anatuhumiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na "kukubali kiasi kikubwa cha hongo" na "kujihusisha na vitendo vya uasherati na wanawake kadhaa". Washirika na jamaa kadhaa wa Zhou pia wanachunguzwa kwa madai ya rushwa.

Mahakama ya ICC imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili Rais Kenyatta

ICC
Mahakama ya Kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai iliyokua inamkabili Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta kutokana na kutokamilika kwa ushahidi.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Katika Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo iliyopo nchini Uholanzi imesema kesi yake haikua na ushahidi wa kutosha wa Kenyatta kuhusika moja kwa moja na mauaji ya maelfu ya Wakenya wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008 akituhumiwa pamoja na William Ruto ambaye ni Makamu wa Rais ambapo maelfu ya wananchi walipoteza maisha.

Maadhimisho ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa shujaa wa Afrika, Nelson Mandela…

Mandela-superJumbo 
Ni mwaka mmoja tangu Mzee Nelson Mandela alipofariki dunia, wananchi wameedhimisha mwaka mmoja toka waondokewe na kiongozi huyo ambaye aliiongoza nchi hiyo kutoka mikononi mwa Makaburu baada ya kufungwa miaka 27 jela.
Maadhimisho hayo yametanguliwa na ibada ya maombi ambapo wamekaa kimya kwa dakika tatu, na kisha kuweka mashada za maua wakiongozwa na wazee waliopigana na makaburu wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi, kumekuwa na upulizaji wa vuvuzela nchini kote, kugonga kengele, ngoma, na kutakuwa na mechi ya mchezo wa kirafiki wa kriketi.
Mandela alikuwa Rais wa kwanza mzalendo kuiongoza Afrika Kusini kwa kipindi cha muhula mmoja wa miaka mitano kuanzia mwaka 1994 hadi 1999 alipoachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
Maduka mengi ya kuchora Tatoo Nchini humo yameripoti ongezeko la watu wanaochora Tatoo za picha ya Mandela.
“… Kimwili hatuko nae lakini kiroho Mandela tuko nae siku zote mpaka mwisho haijawahi kubadilika, Madiba kiroho tuko nae kila siku, najua Madiba anatabasam, Madiba anafurahi kwa sababu yeye ni miongoni mwa familia aliyochagua kuijenga”, alisema Mjane wa Mandela, Grace Machel.
Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, Desmond Tutu katika maadhimisho hayo ametoa wito kwa wananchi Afrika Kusini kuiga mfano wa Mandela.
_79522568_79522567
_79522157_79522156
_79522564_79522158

Alhamisi, 4 Desemba 2014

SERENKUMA AJIUNGA NA KLABU YA SIMBA

 
Mshambuliaji matata wa kilabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dan Sserenkuma aihama kilabu hiyo na kujiunga na Simba SC ya Tanzania 

Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania Simba SC.
Raia huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.
''Nimefurahia miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.

                                                   Dan Sserenkuma

Mchezaji huyo wa kimataifa katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini Daresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi ya Tanzania.
Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.
Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.

MCHEZAJI AFARIKI BAADA YA KUPIGWA KICHWA

Mchezaji Franco Nieto aliyefariki baada ya kupiwa na jiwe kwenye kichwa wakati wa mechi nchini Argentina

Mchezaji wa Argentina Franco Nieto ,mwenye umri wa miaka 33 amefariki baada ya kupigwa kwenye kichwa wakati wa mechi siku ya jumamosi.
Nieto ,nahodha wa kilabu ya kijimbo ya Tiro federal alishambuliwa na genge baada ya mechi kati ya wapinzani wao wa jadi Chacarita Juniors katika mji wa Aimogasta kazkazini magharibi mwa Argentina.
Mechi hiyo ilisimamishwa kwa dakika 15 kabla ya kukamilika baada ya refa kuwapa kadi nyekundu wachezaji wanane kwa kupigana.
Mwaka huu watu 15 wamefariki katika ghasia zilizosababishwa na soka nchini Argentina,Binamu wa Nieto,Pablo Nieto amesema kuwa watu watatu walimzunguka mchezaji huyo alipokuwa akielekea katika gari lake na mkewe na mtoto wao wa mwezi mmoja.
Walimpiga kwa ngumi na mateke kabla ya mmoja ya watu hao kumpiga na jiwe katika kichwa na kumwacha bila fahamu.
Alifanyiwa upasuaji siku ya jumanne lakini akafariki siku ya jumatano.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Fabian Bordon ameviambia vyombo vya habari kwamba watu watatu wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo.
Ghasia zinazosababishwa na soka ni tatizo kubwa nchini Argentina.
Kulingana na shirika moja lilisokuwa la kiserikali Salvemos el Futbol,vifo vinavyosababishwa na ghasia za soka vimeongezeka mwaka huu.
Washukiwa wakuu ni genge la Barras Bravas ambao hudhibiti maneo ya kukalia katika viwanja vya mpira na barabara karibu na viwanja hivyo.
 

AISHI NA MAITI AKITARAJIA ITAFUFUKA

                                                                                 Maiti


Familia moja nchini Canada iliishi na maiti katika chumba cha juu cha nyumba yao kwa miezi sita kwa kuwa waliamini marehemu atafufuka iwapo wataendelea kumuomba mungu,lakini mwili huo ukapatikana baada ya familia hiyo kushindwa kulipa mkopo waliochukua kununua nyumba hiyo.
Kaling Wald mwenye umri wa miaka 50 alipatikana na makosa ya kushindwa kuwaarifu maafisa wa polisi kwamba mumewe alifariki ,kosa ambalo na akahukumiwa kuwekwa katika muda wa majaribio na ushauri,wakili wake alikiambia chombo cha habari cha Reuter siku ya Jumanne.
Peter Wald mwenye umri wa miaka 52 alifariki mnamo mwezi machi mwaka 2013 kwa kile mamlaka inasema ni sababu za kawaida kufuatia maambukizi ya mguu wake yanayodaiwa kusababishwa na ugonjwa wa sukari.
Mkewe Kaling Wald alimwacha kitandani na kufunga chumba hicho katika nyumba yao ya Hamilton ,Ontario ili kuzuia harufu kali iliokuwa ikitoka chumbani humo kuwafikia watu waliokuwa wakiishi nyumbani humo.
Kama vile Yesu alivyomfufua Lazaro baada ya siku ya nne ,pia yeye aliamini kwamba Mungu atamfufua mumewe wakili wa mwanamke huyo alisema.

Binti aliyeongoza Matokeo ya darasa la saba kuozeshwa kwa mahari ya kilo 2 za sukari

girl
Pamoja na Serikali kuendelea kupiga vita wazazi kuwaoza mabinti zao wakiwa bado wadogo lakini bado kuna baadhi ya makabila hapa nchini wameendeleza utamaduni huo kwa kuwaoza mabinti zao sababu kubwa ikitajwa kuwa ni tamaa za kutaka kujilimbikizia mali.
Lakini kwa msichana huyu wazazi wake wameonekana kutoijali hata ile mali waliyopewa kwani wameweza kumwozesha binti yao wa kike kwa mahari ya kilo mbili za sukari toka kwa mfugaji wa kabila la kimasai.
Gazeti la NIPASHE limeripoti kuwa mmoja wa wanafunzi walioongoza darasa wa Taifa wa Darasa la saba mwaka huu mwenye umri wa miaka 16 anadaiwa kuozwa kwa mwanaume mwenye miaka 50 baada ya wazazi wake kupewa sukari kilo mbili kama mahari.
Kutokana na hali hiyo mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketeji Mkoani Kilimanjaro NAFGEM umefanya jitihada za kumuokoa pamoja na wanafunzi wengine15 waliotaka kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa ngariba.
Msichana huyo wa miaka 16 wa kabila la kimasai ambaye jina lake limehifadhiwa baada ya kufaulu mtihani huo kwa asilimia kubwa huku akitajwa kuwa miongoni mwa wasichana waliofanya vizuri aliozeshwa kwa mwanaume mmoja ambaye ni mfugaji wa kabila hilo.
Meneja Mpango wa mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketaji Mkoani Kilimanjaro Honoratha Nasua alitoa taarifa za kuolewa kwa binti huyo walizipata huku wanafunzi wengine 15 wakisubiri tarehe ya kufanyiwa ukeketaji ili waozeshwe baada ya tendo hilo.
Alisema suala la mwanafunzi huyo aliyeozeshwa limefikishwa katika dawati la jinsia la Polisi Wilayani Siha kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria.
Alisema wazazi wa mwanafunzi huyo wamechangia kudidimiza maendeleo ya mtoto wao kwa kukubali aolewe na kubuni mbinu mpya ya kukeketa watoto wachanga ili kukwepa mkono wa dola na vyombo vya wanaharakati.
Mtandao huo wa kupinga ukeketaji unaendelea na shughuli zake katika Wilaya hiyo ikishirikiana na Shirika la kimataifa la Elimu kwa ufadhili wa Shirika la misaada la kimataifa la Marekani USAID kupitia mpango wa pamoja wa TUWALEE.

Yule mama aliyejiuzulu kwa kukosoa mavazi ya watoto wa Obama kumbe bado anafuatiliwa?

sasha-malia-2-477 
Moja ya story ambazo zilichukua uzito wa juu katika vyombo vya habari wiki iliyopita ilikuwa ni kitendo cha yule mama mfanyakazi wa Chama cha Republican Marekani, Elizabeth Lauten ambaye alikuwa kitengo cha Mawasiliano kukosoa mavazi ya watoto wa Obama bado ni story inayoendelea kuzungumziwa.
Mama huyo aliwaponda Sasha na Malia kuwa wamekosa ustaarabu kutokana na kuvalia sketi fupi katika hafla ya chakula katika Ikulu ya White House, pia alisema kuwa watoto hao ni kama hawakuwa na nyuso za furaha kuwa katika hafla hiyo, ambapo baada ya kushambuliwa na watu kwenye ukurasa wake wa Facebook aliomba radhi, na baadaye akajiuzulu.
141130152136_turkey_640x360_getty
Leo ni siku ya nne tangu amejiuzulu lakini story ni kwamba bado ameendelea kufuatiliwa na vyombo habari, huku wengine wakipiga kambi nyumbani kwa wazazi wake kuchunguza vitu mbalimbali ikiwemo rekodi ya maisha yake ya utotoni ambapo watu kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa kwa kusema hiyo haikuwa ‘big deal’ ya kufanya vyombo vya habari kumfuatilia kiasi hicho.

Jumanne, 2 Desemba 2014

NI MSANII ANAEKUJA VIZURI KUTEKA SANAA YA MUZIKI TANZANIA TOKEA KILIMANJARO

Ni moja kati ya wasanii waliofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Tanzania kwa mwaka 2014 toka Kilimanjaro.Ramjey ndo jina lake katika sanaa akiwa amemshirikisha Rita ngoma yake inakwenda kwa jina la Sijajua kosa langu ambayo imefanywa na producer Malwo kutoka studio ya Sunlight.Ni msanii ambae amejaaliwa sauti nzuri na anaitendea haki kwa ngoma kali aliyoiachia hivi karibuni.Ili kuiskiliza ngoma ya huyu mkali toka Kilimanjaro mkoa ambao haubahatishi katika muziki DOWNLOAD hapa chini ili uweze kusikiliza.


Hii ni kuhusu matokeo ya zoezi la upimaji wa kilevi kwa madereva wa mabasi Ubungo

20141202_131149
Lile zoezi ambalo lilianzishwa na Jeshi la Polisi Tanzania kukagua madereva wanaoendesha mabasi ya abiria kwenda mikoani kama wanatumia kilevi leo limefanyika kwa ghafla katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1 imesema zoezi hilo limetoa majibu kwamba madereva wamekuwa na uelewa juu ya athari za matumizi ya kilevi wakiwa wanaanza safari.
Unaweza kuisikiliza hapa taarifa hiyo niliyokurekodia wakati habari hiyo ikirushwa hewani.

BARNES:GERRAD BADO MZURI KWA LIVERPOOL

Steven Gerrard bado ana kiwango cha juu kuendelea kuitumikia Liverpool

Winga wa zamani wa Klabu ya Liverpool John Barnes anaamini kiungo na nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard, bado ni mzuri vya kutosha kuendelea kuitumikia liverpool
"Katika hatua hii ya kazi yake, bado ni bora kabisa na uzuri wa kutosha kwa ajili ya Liverpool bado," Barnes alisema.
Barnes alitumia misimu 10 katika uwanja wa Anfield kabla ya kuondoka na kujiunga na Newcastle United katika umri ambao anao Gerrard hivi sasa.
Pamoja na ufanano wa umri ambao Barnes aliihama liverpool winga huyo anaimani Gerrard ana nafasi yakuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka atakapostaafu soka.
"Bila shaka tunajua ubora wa Gerrard ulivyokua nyuma, na tunajua nini huwatokea wachezaji wengi wanapofika mwisho wa kazi zao,bado ni mchezaji muhimu sana kwa klabu ya Liverpool”.
tayari liverpool kupitia meneja wake Brendan Rodgers imetangaza kumpa ofa ya mkataba mpya. Steven Gerrard utakao muwezesha kumalizia kipaji chake kwa majogoo wa jiji la London.

Aliyewakosoa Sasha na Malia ajiuzulu

Sasha na Malia walikosolewa kwa kuvalia sketi fupi mbele ya umati katika White House

Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.
 
Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari

Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.
 Sasha na Malia ni miongoni mwa vijana wadogo sana kuwahi kuwa katika ikulu ya White house


Mwanamke huyo akiomba msamaha, alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha mwenendo wangu, '' alisema Lauten.

MKE WA KIONGOZI IS AKAMATWA

                      Kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdadi


Vikosi vya usalama nchini Lebanon vimemkamata mkewe kiongozi wa kundi la wapiganaji wa kiislamu la IS Abu Bakr al-Baghdadi karibu na mpaka na Syria na mwanawe mvulana.
Jeshi linasema kuwa Mkewe Baghdadi alikamatwa pamoja na mwanawe ingawa majina yao hayajatolewa. Walikamatwa na wakuu wa ujasusi baada ya kuingia Lebabon siku kumi zilizopita.
Jarida la al-Safir liliripoti kuwa mkewe Baghdadi anahojiwa katika ofisi za waizara ya usalama nchini Lebanon.
Mnamo mwezi Juni, Baghdadi alitajwa kama kiongozi wa kundi hilo katika maeneo ya Syria na Iraq ambayo yanadhibitiwa na IS.
Mwezi jana kundi hilo lilikannusha madai kuwa kiongozi huyo aliuawa au kujeruhiwa, katika shambulizi la angani lililofanywa na majeshi ya Marekani, mjini Mosul.
Kundi lenyewe lilitoa kanda ambapo lilisema utawala wao unapanuka na kutoa wito kwa wapiganaji wa jihad kujitolea mhanga.
Jarida lililoripoti kukamatwa kwa mkewe Baghdadi, limesema kuwa maafisa wa usalama walikuwa wameiweka operesheni yao kama siri kubwa kiasi kwamba hakuna aliyekuwa na taarifa kuhusu operesheni yenyewe.
Mwandishi wa BBC Jim Muir, ambaye yuko, anasema kuwa kukamatwa kwa mkewe Baghdadi na mwanawe kutawaweka katika hali tatanishi ambayo inaendelea kuibuka Lebanon.
Kundi la IS pamoja na kundi lengine la jihad al-Nusra linawazuilia wanajeshi 20 wa Lebabon kama mateka.

Al Shabaab waua 36 Mandera,Kenya

 
                                 Wapiganaji wa Al Shabab 


Kundi la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya.
Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia.
Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu.
Inaarifiwa kuwa wafanyakazi hao walipigwa risasi wakiwa katika mahema ya. Walioshuhudia shambulizi walisema kwamba wapiganaji hao waliwatenga waisilamu na wakristo huku wakiwachinja baadhi, na kuwapiga risasi wlaiosalia.
Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya.
Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera.
 
     Watu wengine 26 waliuawa na wapiganaji hao mjini Mandera wiki iliyopita 

Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab wamekiri kuhusika na mauaji hayo.
Mkuu wa Polisi eneo hilo, amesema bado wanafuatilia tukio hilo.
Katika tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini Kenya kufuatia mlipuko katika klabu moja ya usiku katika mji wa Wajir kaskazini mwa Kenya.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi wa Wajir, Frederick Sishia, shambulio hilo limefanyika saa mbili usiku na kuua mtu mmoja na watu wengine wanne wamejeruhiwa.
Washambuliaji hao walitumia magruneti na silaha nyingine za kijeshi kufanya shambulio hilo.
Wiki iliyopita watu wengi waliuawa eneo la Mandera kaskazini mwa Kenya.
Kenya imejikuta ikilengwa na mashambulio ya kigaidi tangu majeshi yake yapelekwe nchini Somalia kukabiliana na wapiganaji wa Al Shabab. Mbali na miji ya kaskazini mwa Kenya kushambuliwa kila mara, miji mikubwa nchini humo ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikilengwa na mashambulio ya kigaidi.

Jumatatu, 1 Desemba 2014

Man city wazidi kupanda

 
              Wachezaji wa Klabu ya Man city 
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema ushindi wa timu yake dhidi ya Southampton unadhihirisha kikosi chake ni imara kuweza kukabiliana na Chelsea katika mbio za kuusaka ubingwa wa ligi ya England.
Kwa ushidi wa mabao 3-0 dhidi Southampton siku ya jumapili, Machester city imepanda hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi sita nyuma ya vinara Chelsea.
Pellegrin amewamwagia sifa kem kem wachezaji wake kwa kuwa na moyo wa kujituma wakiwa uwanjani hali iliyozaa matunda hayo.

Obama na vurugu za Marekani

                                                             Barack Obama

Rais Barack Obama wa Marekani na baraza lake leo anatarajiwa kuwa na majadiliano kuhusiana na machafuko yanayoendelea katika miji ya Ferguson na Missouri kutokana na kuuawa kwa kijana mweusi na polisi wa kizungu.
Mkutano huo utalenga namna ya kuleta hali ya kuaminiana kati ya polisi na jamii na pia kuangalia vyombo vya kupitia mipango ya serikali kuendeleza hali ya amani.
Meya wa jimbo la Ferguson ametangaza siku ya jumapili polisi Darren Wilson alitangaza kujiuzuru hatalipwa mafao yake kama sehemu ya adhabu kwa kitendo alichokifanya cha mauaji.
Hatua iliyofikiwa ya kupitisha kutomfungulia mamshtaka ndiko kulikoshuka ghasia katika jimbo la Ferguson na katika maeneo mengine ndani ya Marekani.

Jumapili, 30 Novemba 2014

FIFA:Madai mapya ya ufisadi yazuka

 
Rais wa FIFA Sepp Blatter akimkabidhi rais wa Urusi Vladmir Putin Haki za kuandaa dimba la dunia la mwaka 2018 


Madai zaidi yameibuka kuhusu ufisadi uliofanyika wakati wa shughuli ya kuwatafuta waandalizi wa kombe la dunia la mwaka 2018 na 2022.
Nafasi hizo zilichukuliwa na Urusi pamoja na Qatar. Gazeti la Sunday Times nchini Uingereza limesema kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin alihusika pakubwa wakati nchi yake ilipokuwa ikitafuta nafasi hiyo na hata alimuomba rais wa FIFA Sepp Blattter kuisaidia kupata kura.
   
Rais wa FIFA Sepp Blatter akiikabidhi Qatar mkataba wa kuandaa kombe la dunia la mwaka 2022

Pia kuna madai kuwa nchi ya Qatar ilitumia ushawishi wake katika sekta ya gesi kupata kura kupitia kandarasi za kibiashara.
Urusi na Qatar zimekana kuhusika kwenye vitendo hivyo na ziliondolewa lawama na shirikisho la soka duniani FIFA hivi majuzi.

Man U na Arsenal zawika,Chelsea yazuiwa

           Mchezaji wa chelsea Wiilian akikabiliana na mwenzake wa Sunderland 

Mkufunzi Gus Poyet aliihangaisha timu ya Chelsea na kuwajaribu viongozi hao wa Ligi kupitia mchezo mzuru wa timu yake Sunderland.
Chelsea ilishindwa kuliona lango la Sunderland kupitia ngome mahsusi ya Sunderland iliowazuia washambuliaji wake.
Shambulizi kali ambalo nusra liiweke Chelsea kifua Mbele ni lile lakKiungo wa kati Willian ambalo liligonga chuma cha goli na kutoka nje.
Hatahivyo Mshambuliaji wa Sunderland pia naye alipiga mkwaju mkali uliogonga chuma cha goli la Chelsea huku Sunderland ikidhibiti safu ya kati na kuimarisha mashambulizi yake katika ngome ya Chelsea.
 
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger afurahi baada ya timu yake kuichapa West Brom 1-0 
Mchezo huo ulikamilika na sare ya bila kwa bila na kuifanya Sunderland kuwa timu ya kwanza kuwazuia viongozi hao wa Ligi kufunga tangu msimu huu uanze.
Katika matokeo mengine Arsenal ilizuia kupoteza kwa mara ya tatu mafululizo pale walipoishinda West Brom ugenini.
The Gunners kama wanavyojulikana walianza mechi hiyo wakiwa na alama za chini zaidi baada ya kucheza mechi 12 katika kipindi cha miaka 32,lakini cichwa kizito cha mshambuliaji Danny Welbeck, kilihakikisha vijana wa Arsene Wenger wanatia kibindoni alama tatu.
        Wayne Rooney afurahia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya timu ya Hull City 
Katika uwanja wa Old Trafford,bao la Robbin Van Persie Robin liliimarisha ushindi wa Manchester United dhidi ya Hull City na kuzima midomo ya wale waliokuwa wakijiuliza maswali mengi kuhusu hali ya mchezaji huyo msimu huu.
Miongoni mwa wakaosoaji wake ni kocha Louis Van Gaal ambaye aliyemuorodhesha mshambuliaji huyo katika mechi hiyo licha ya kudai kwamba alikuwa na mchezo m'baya wakati wa mechi kati ya Arsenal na Manchester wikendi iliopita.
Manchester United ilipata ushindi wa mabao 3-0 kupitia wachezaji wake Chris Smalling na nahodha Wayne Rooney.
katika matokeo mengine
Burnley 1 - 1 Aston Villa
Liverpool 1 - 0 Stoke
QPR 3 - 2 Leicester
Swansea 1 - 1 Crystal Palace
West Ham 1 - 0 Newcastle

ESCROW:Spika adaiwa kuwalinda washukiwa

 
                     Spika wa bunge la Tanzania Anne Makinda 
Speaker wa Tanzania Anne Makinda ameshtumiwa kwa kujaribu kuwatetea wale wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi ya Escrow.
Kulingana na wachambuzi,wasomi na wataalam wa sheria hatua yake ya kujenga mazingira ya kuwapendelea washukiwa huenda ikasaidia kuwalinda watu hao.
Wakili maarufu mjini Daresalaam Sylvanus Sylivand ameliambia gazeti la the Citizen kwamba spika makinda alitarajiwa kufuata mfano mzuri uliowekwa na wenzake katika kashfa za awali ambapo bunge lina uwezo wa kuwashinikiza mawaziri na waziri mkuu kujiuzulu.
Ni wazi kwamba bunge linaweza kuishauri serikali kuwachukulia hatua viongozi wanaoshukiwa lakini si lazima kwamba rais afuate agizo hilo.
Kulingana na Sylivand,ni wazi kwamba kuna kitu kinachofichwa ili kuendesha ajenda tofauti ambayo itasadia aibu iliopata serikali.
  
                                           Bunge la Tanzania 


Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma Paul Loisulie amesema kuwa bunge sharti lichukue hatua kama taasisi.
''Kile ambacho kimetokea bungeni kuna uwezekano mkubwa kitaligawanya bunge na wananchi.''.
Inaonekana kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wanajaribu wawezalo kuwatetea viongozi wanaoshukiwa bila kujali maslahi ya raia walio masikini.
Julius Mtatiro wa Chama cha Civic Front amesema kuwa CCM inataka kuwalinda viongozi wake wakuu ili raia wasielewe kuhusu kilichotokea baada ya Spika Makinda kuwataka baadhi ya washukiwa hao kupendekeza hatua ambazo zingefaa kuchukuliwa dhidi yao.
Kulingana na Profesa Kitila wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Wabunge wana uwezo wa kuwaweka katika mizani watu watatu pekee ,rais,waziri mkuu na Spika na kile kilichokuwa kikendelea bungeni ni fursa ya wananchi kufikiria sana kabla ya kuipitisha katiba mpya.

Walichokisema Wabunge Kafulila, Peter Msigwa, Aeshi Hilary na Maige kuhusu maamuzi ya Bunge jana

news0
Kikao cha Bunge la Tanzania kilichoahirishwa siku ya jana Novemba 29 ni moja ya vikao ambavyo vilivuta hisia za watu wengi na kutengeneza historia nyingine mpya kutokana na mjadala wa ishu ya Escrow, baada ya kikao hicho kuahirishwa Wabunge Ezekiel Maige, Aeshi Hilary, David Kafulila na Mchungaji Peter Msigwa walizungumzia kuhusu maamuzi ya Bunge hilo.
…Tumekuwa na Bunge la kipekee sana katika muda wangu wa kuwa Mbunge karibu miaka nane sasa, hii ni experience yangu ya kwanza kuwa na kipindi kigumu kama hiki. Bunge limekuwa kwenye mtihani wa ama kuamua kulinda viwango vyake vya utendaji wa miaka yote au kuamua kuwa na viwango tofauti…” —Ezekiel Maige.
… Niwaombe Watanzania wawe wavumilivu kila kitu kina wakati wake na muda wake… Nilipongeze Bunge, nipongeze kamati ya usuluhishi vilevile nimpongeze Waziri Mkuu kwa kukubaliana na haya, ninaamini Serikali itachukua hatua zake…”– Aeshi Hilary.
…Niliamini siku zote kwamba kuna makosa yamefanyika katika utoaji wa fedha zile na chunguzi za CAG, PCCB, na hatimaye kamati ya PAC zimeonyesha hivyo na hatimaye Bunge limeweza kuchukua hatua hii. Kuna changamoto nyingi katika kupambana na mambo kama haya, kuna vitisho, kudhalilishwa mimi niliitwa ‘tumbili’ na kuna watu walitishia kuniua, lakini yote kwa ujumla wake ni changamoto katika kupambania yale ninayoamini…” –David Kafulila.
… Tumetimiza wajibu wetu kuishauri Serikali, tumeona watu wengine hawakutimiza wajibu wao… Upande wetu wa upinzani tuling’ang’ania kwamba watu wawajibike, niwasihi wananchi tuendelee kushirikiana kwa sababu mwisho wa siku hii ni nyumba ya kwetu sote mtu yeyote asiyetimiza wajibu wake lazima abebe mzigo wake …”—Mchungaji Peter Msigwa.

Maneno 6 ya Davido baada ya ushindi wa Diamond Platnumz Channel O 2014.

Davido 12 
Ushindi wa tuzo tatu za Channel O 2014 alizochukua Mtanzania Diamond Platnumz umekua mkubwa sio tu kwa Tanzania bali Afrika na kona zake ambapo miongoni mwa walioandika baada ya Diamond kushinda ni Davido.
Msanii huyu wa Nigeria ambae alifanya remix ya number one ya Diamond aliandika kwenye page yake ya instagram >>> TANZANIA STAND UP! HE DID IT na kisha akammention Diamond Platnumz.
Kwenye post hii ya Davido ambae hakupata tuzo yoyote ya Channel O japo alikua anawania, imepata likes zaidi ya elfu kumi na nne kutoka kwa followers wake ambao ni zaidi ya laki nne huku comments zikiwa ni zaidi ya mia saba.
Davido on Diamond
Davido 13

Jumamosi, 29 Novemba 2014

DIAMOND PLATNUMZ ANYAKUA TUZO 3 ZA CH0AMA14

 
Tar 29 Noember ni siku ambayo imewekwa historia kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva baada ya Diamond Platnumz kuchukua tuzo tatu za chanel O, pia ni historia kwa Afrika nzima.
Diamond alikua ametajwa kwenye vipengele vinne. Vipengele hiyo ni pamoja na Most Gifted East Video, Most Gifted Afro Pop video na Most Gifted Newcomer.
Kwenye tuzo hizo Diamond amefanikiwa kuwapiku wasanii nguli wa Afrika  wakiwemo Iyanya, Daido, Flavor, Mafikizolo na Sauti Sol.

 "TANZANIA STAND UP! HE DID IT! @ diamondplatnumz", amepost Davido